Connect with us

Kitaifa

CCM yamtimua uanachama Balozi Karume

Unguja. Hatimaye CCM Zanzibar imemfuta uanachama kada wake, Balozi Ali Karume na kumtaka arejeshe kadi ya chama hicho.

 Hatua hiyo imefikiwa zikiwa zimepita siku 23 tu tangu Balozi Karume alipopewa barua ya onyo Juni 15, kabla ya juzi kuibuka tena akisisitiza kauli zake kwamba hakuna demokrasia ndani ya CCM.

Kabla ya hatua hiyo, Karume alihojiwa na kamati ya maadili ya CCM tawi la Mwera, akahojiwa na kamati ya maadili ya CCM Jimbo la Tunguu na alihojiwa na kamati ya maadili ya CCM Wilaya ya Kati na kupewa barua ya onyo akiwekwa chini ya uangalizi wa miezi mitatu.

Uamuzi wa kumfukuza uanachama umetolewa leo Juni 8, 2023 saa 9:00 usiku na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja chini ya Katibu wa Mkoa huo, Amina Mnacho.

Akitangaza uamuzi wa kikao hicho Katibu Mwenezi wa CCM mkoa huo, Ali Timamu Haji amesema umefikiwa baada ya kumjadili na kupokea mapendekezo kutoka vikao vya chini kuhusu mwenendo na tabia ya mwanachama huyo.

“Tumepokea mapendekezo kutoka vikao mbalimbali vya chini na tumevipitia na sisi kama chama Mkoa kwa mujibu wa katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2022 ibara ya 89 (4) Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa inatupa nguvu hiyo,” amesema.

Amesema ibara ndogo ya 14 (14) inaelekeza kuwa kumuachisha au kumfukuza uanachama mwanachama yoyote endapo itathibitika kuwa endapo tabia na mwenendo wake vinamuondolea sifa za uanachama na mwanachama anayefukuzwa anaweza kukata rufaa kwa kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

“Kwa maana hiyo baada ya kupewa nguvu na katiba na kupitia yote kutoka ngazi za chini Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa imeridhia kwa kauli moja kwamba kutokana na kauli na vitendo vya mwanachama huyu, tumekubaliana kumuachisha uanachama wa CCM kadi nambari C000/2809/993/1 iliyotolewa Machi 17, 2022,”

Hatua ya kumfukuza uanachama inakuja baada ya chama hicho kumpa onyo kutoka na kauli zake zake akidaiwa kukidhalilisha chana na kuwatukana viongozi wakuu hadharani.

Kabla ya hatua hiyo, kada huyo alihojiwa na kamati ya maadili ya CCM tawi la Mwera, akahojiwa na kamati ya maadili ya CCM Jimbo la Tunguu na alihojiwa na kamati ya maadili ya CCM Wilaya ya Kati na kupewa barua ya onyo akiwekwa chini ya uangalizi wa miezi mitatu.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi