Connect with us

Kitaifa

Asilimia 70 waenda kidato cha tano, wasichana safi

Dodoma. Wanafunzi 188,128 waliokidhi vigezo wamechaguliwa na kupangiwa kujiunga na kidato cha tano katika shule na vyuo vya fani mbalimbali.

Wanafunzi 122,908 wakiwemo wasichana 62,731 na wavulana 60,177 wamepangiwa katika shule 519 za sekondari za bweni za kidato cha tano huku wanafunzi 58,298 wakiwemo wasichana 18,166 na wavulana 40,132 sawa na asilimia 31 wamepangiwa kujiunga kwenye kozi za stashahada katika vyuo vya kati.

Takwimu hizi ni sawa na kusema wanafunzi saba kati ya 10 waliofaulu wamepangiwa kujiunga na kidato cha tano huku wengine watatu kati ya 10 wakipangiwa vyuo vya fani tofauti.

Wanafunzi 1,878 wakiwemo wasichana 1,097 na wavulana 781 wamepangiwa katika shule za sekondari maalumu nane ambazo ni Kilakala,Mzumbe,Ilboru, Kisimiri,Msalato,Kibaha,Tabora Boys na Tabora Girls.

Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022 yanaonyesha kuwa watahiniwa 192,348 walipata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu ambapo kati ya hao Tanzania Bara walikuwa watahiniwa 188,128 wakiwemo wasichana 84,509 na wavulana 103,619.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Angelah Kairuki alisema wamezingatia takwimu za matokeo ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2022 kutoka Tanzania Bara.

Alisema wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka katika shule za Serikali,binafsi,watahiniwa wa kujitegemea waliofanya mtihani chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na vyuo vya maendeleo ya wananchi.

Alisema wanafunzi 129,830 wakiwemo wasichana 66,343 na wavulana 63,487 sawa na asilimia 69 ya wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari za kidato cha tano 540 zikiwemo shule mpya 29 zinazoanza mwaka 2023.

Aidha, takwimu zinazidi kuwaweka wasichana kuwa vinara katika elimu ya sekondari na msingi ambapo katika matokeo haya kati ya wanafunzi waliochaguliwa kidato cha tano asilimia 51 ni wasichana huku asilimia 49 wakiwa wavulana.

Waziri Kairuki alisema wanafunzi 1,878 wakiwemo wasichana 1,097 na wavulana 781 wamepangiwa katika shule za sekondari maalum nane ambazo ni Kilakala, Mzumbe, Ilboru,  Kisimiri, Mlasato, Kibaha, Tabora Boys na Tabora Girls.
Alisema wanafunzi 122,908 wakiwemo wasichana 62,731 na wavulana 60,177 wamepangiwa katika shule 519 za sekondari za bweni za kidato cha tano.
Waziri Kairuki alisema wanafunzi 5,044 wakiwemo wasichana 2,515 na wavulana 2,529 wamepangwa katika shule 11 za sekondari za kutwa za kidato cha tano.

Waliochaguliwa vyuoni

Waziri Kairuki alisema wanafunzi 58,298 wakiwemo wasichana 18,166 na wavulana 40,132 sawa na asilimia 31 wamepangiwa kujiunga kwenye kozi za stashahada katika vyuo vya kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTVET).

Alisema wamechaguliwa kwa mchanganuo wa wanafunzi 1,645 wakiwemo wasichana 646 na wavulana 999 wamechaguliwa kujiunga vyuo vya ualimu ngazi ya stashahada ya Sayansi,Hesabu na Tehama.

Alisema wanafunzi 1,877 wakiwemo wasichana 757 na wavulana 1,120 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika vyuo vinne (4) vya ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi Arusha (ATC),Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST) na Chuo cha Usimamizi na Maendeleo ya Maji (WDMI).

Waziri Kairuki alisema wanafunzi 1,842 wakiwemo wasichana 943 na wavulana 899 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya afya ngazi ya Stashahada.

Alisema wanafunzi 52,934 wakiwemo wasichana 15,820 na wavulana 37,114 wamechaguliwa kujiunga kwenye kozi mbalimbali zikiwemo za kilimo,ufugaji,utawala, biashara na katika vyuo vya kati mbalimbali nchini.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi