Connect with us

Kitaifa

Sintofahamu mgomo Kariakoo

Dar es Salaam. Licha ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na wafanyabiashara katika soko la Kariakoo jana Mei 15, 2023 na kuahidi kuzipatia ufumbuzi changamoto zao, bado wafanyabiashara hao wamegomea agizo hilo Licha ya wachache kuonekana kutii agizo.

Ambapo Mwananchi asubuhi ya leo hadi saa 4.30 imeshuhudia maduka yakiwa yamefungwa na wafanyabiashara wakiwa wamesimama katika vikundi wakijadili hatma yao.

Jana wafanyabiashara hao walifunga maduka yao kwa saa 12 wakishinikiza kuonana na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye wamemtaja kwamba ndiye mtatuzi wa kero zao.

Miongoni mwa kero walizotaja wafanyabiashara hao ni kamatakamata inayofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Sheria mpya ya usajili wa stoo pamoja na kero zinginezo.

Jana Amos Makalla aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alifika sokoni hapo na kuwaomba wafanyabiashara kusitisha mgomo na wangeonana na Waziri Mkuu Majaliwa siku ya Alhamis jijini Dodoma lakini wafanyabiashara hao walidai wamechoshwa na maagizo ya kisiasa.

Kauli hiyo ilipingwa na Wafanyabiashara hao wakimtaka Waziri Majaliwa afike sokoni hapo na awasikilize, hata hivyo Majaliwa alifika sokoni hapo na kuwaomba wafanyabiashara kusitisha mgomo huku akiondoa kikosi kazi cha TRA pamoja na kukemea watumishi wanaodharau matamko ya viongozi.

“Hakuna kiongozi wa serikali anatakiwa kumdharau kiongozi wa juu, Rais na Makamu wa Rais wanaposimama kutoa maagizo sisi wa chini tunatekeleza mbiombio

TRA Rais amesema kodi ya miaka mitano nyuma achaneni nayo anzia mitano kwenda mbele wewe unamdai mfanyabiashara wa Kariakoo barua hiyo ni dharau ya hali ya juu.Natamani nimjue nani huyo”emesema.

Kauli hiyo iliambatana na ombi la Waziri Mkuu kuwataka wafanyabiashara hao kusitisha mgomo na kuitikiwa lakini leo hali ni tofauti kwani bado wafanyabiashara hao wanaendelea na mgomo.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi