Connect with us

Kitaifa

Geita kutumia Sh1.8 bilioni kupunguza msongamano shuleni

Geita. Serikali imetoa zaidi ya Sh1.8 bilioni kujenga shule tatu za msingi katika Kata ya Buhalahala Halmashauri ya mji wa Geita kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule za Mwatulole na Nguzo Mbili zenye wanafunzi zaidi ya 10, 000.

Ofisa Elimu Msingi (Elimu maalum) Halmashauri ya Mji Geita, Zunaeda Alphonce amesema shule hizo zitakazokuwa za mfano zitakuwa na vyumba 21 vya madarasa, matundu 42 ya vyoo, jengo la mawasiliano na teknolojia na nyumba pacha za walimu.

Akitoa taarifa wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule hiyo ya mfano kwa gharama ya Sh800 milioni, Zunaeda amesema mradi huo tayari umefika asilimia 60 ya utekelezaji.

Amesema kupitia mpango huo wa kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani, Serikali pia imetoa zaidi ya Sh900 milioni kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya kupunguza msongamano katika shule za Nguzo Mbili na Mwatulole zenye wanafunzi zaidi ya 10, 000.

‘’Kila shule imepokea Sh450 Milioni kupitia mradi wa Boost kutekeleza mradi huo,’’ amesema Zudaeda

Amesema utekelezaji wa mradi huo uko katika hatua za awali ya kusafisha maeneo ya mradi na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, mwaka huu.

Akizungumzia miradi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella amesema ni dhamira ya Serikali kuendelea kuboresha mazingira na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika shule zote za umma ili kuzifanya kuwa bora na rafiki kwa walimu na wanafunzi.

Katika ziara hiyo, Shigela pia ametembelea shule mpya ya sekondari Fazilibucha yenye wanafunzi 250 ambako alikagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala kwa gharama ya Sh155 milioni kupitia fedha za Mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, (Tasaf).

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi