Connect with us

Kitaifa

Ripoti: Ushuru kwenye ‘bando’ la intaneti waongezeka Tanzania

Dar es Salaam. Ripoti ya robo mwaka unaoishia Machi 2023 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaonyesha gharama za ushuru wa bando la intaneti zimeongezeka ikiliganishwa na kipindi kama hiko Machi 2022.

Machi 2022 kwa kila MB moja ushuru uliokuwa unakatwa ni shilingi mbili ambayo imeongezeka hadi kufikia Sh2.09 Machi 2023.

Aidha, ripoti hiyo inaonyesha gharama za ushuru wa bando la dakika na ujumbe mfupi umepungua Machi 2023 ikilinganishwa na Machi 2022.

“Gharama za ushuru wa bando la dakika za kupiga mitandao yote ni Sh6.37 kwa kila dakika Machi 2023 ikilinganishwa na shilingi tisa Machi 2022. Kupiga ndani ya mtandao mmoja Machi 2022 ilikuwa inatozwa shilingi nane kwa kila dakika imepungua hadi kufika Sh4.66,” imesema ripoti hiyo.

Aidha kwa upande wa ujumbe mfupi Machi 2022 ulikuwa unatozwa shilingi tatu kwa kila mmoja huku ikishuka hadi Sh1.34 kwa kila ujumbe mmoja.

Mbali na gharama hizo, pia ripoti hiyo inaonyesha laini za simu zinazotumika nchini zimeongezeka kutoka milioni 55.3 Machi 2022 hadi milioni 61.9 Machi 2023 sawa na ongezeko la asilimia 11.9.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi