Kitaifa
Rais Mwinyi aagiza mishahara ilipwe mapema wajiandae na Eid
Unguja. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameagiza malipo ya mishahara ya wafanyakazi wa Serikali kufanyika mapema kwa ajili ya matayarisho ya sikukuu ya Eid El Fitr.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu leo Jumapili Aprili 16, 2023, inasema Rais Mwinyi ameagiza malipo hayo yaanze kufanyika Aprili 14, mwaka huu.
Kwa mujibu wa tamko la Rais, hatua hiyo inalenga kuwapa muda wa kutosha wafanyakazi serikali kufanya maandalizi ya sherehe hizo.
Sherehe hizo zinatarajiwa kuangukia kati ya siku ya Ijumaa au Jumamosi (Aprili 21 au 22, 2023) kutokana na kuandama kwa mwezi na kuashiria mwisho wa mwezi.
“Pia Rais Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyakazi wa Serikali kwa ushirikiano wao wakati wote wa ibada tangu kuandama kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan,”