Uncategorized
Rais Samia avunja Bodi ya TRC, atengua uteuzi wa TGFA
Dar es Salaam. Wiki moja baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Rais Samia Suluhu Hassan ameanza kuchukua hatua.
Ripoti ya CAG iliwasilishwa bungeni jijini Dodoma Alhamisi, Aprili 6, 2023 ikihusisha madudu lukuki yaliyofanywa na taasisi za umma.
Katika hotuba yake wakati akipokea ripoti hiyo, Rais Samia alikemea vikali watendaji wasio waadilifu, akisisitiza walioshindwa wampishe.
“Hatuwezi kwenda hivyo na nadhani hao wanaopokea hizo invoice wakazileta Serikalini kwa raha zao kabisa, watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa wangelifanyia kazi huko huko,” alisema Rais Samia akikemea utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji wake.
Hatimaye leo Aprili 9, 2023 Mkuu huyo wa nchi ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kutengua nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Mhandisi John Nzulule.
Kulingana na ripoti hiyo ya CAG ya 2021/22, TRC katika mwaka wa fedha 2020/2021, lilipata hasara ya Sh22.8 bilioni huku mwaka 2021/2022 ikipata hasara ya Sh31.29 bilioni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa Rais amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi kuwaelekeza Makatibu Wakuu wa Watendaji Wakuu kusoma ripoti hiyo, kujibu na kuzifanyia kazi hoja zote.
“Watendaji wote watakaobainika kuhusika na uzembe au ubadhilifu wachukuliwe hatua za kisheria,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Bodi ya Wakurugenzi ya TRC, ilikuwa ikiongozwa na Mwenyekiti Profesa Wajanga Kondoro, Katibu wa Bodi hiyo alikuwa Masanja Kadogosa, huku wajumbe ni London Kibugula, Dk Jabir Bakari na Benjamin Mbimbi.
Wajumbe wengine ni Lilian Ngilangwa, Joseph Salema, Juma Kijavara na Pe