Connect with us

Kimataifa

Odinga awaonya polisi wasithubutu kuzuia maandamano

Kenya. Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amewaonya polisi kwamba wasisubutu kumkamata leo Jumatano 27, 2023, huku akiahidi kuendelea na maandamano dhidi ya serikali ambayo yamepigwa marufuku.

Polisi nchini humo wameweka doria ili kuzuia maandamano ya kitaifa ambayo yamepangwa kufanyika mara mbili kila wiki.

Shirika la Habari la Uingereza la BBC Swahili limeeleza kwamba, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kithure Kindiki jana Jumapili alitangaza kwamba serikali itatunga sheria mpya ya kuweka vikwazo kwa maandamano, huku akisema polisi hawatavumilia kufanyika maandamano yenye ghasia.

Kindiki alitoa taarifa baada ya Inspekta Jenerali wa Polisi, Japhet Koome kuwaonya viongozi wa upinzani kwamba watakamatwa kwa kuwa hajatoa ruhusa kwa maandamano hayo kufanyika.

Baadhi ya wanasiasa wa Muungano wa Kenya Kwanza, wamemtaka kiongozi wa upinzani Raila Odinga kumpa Rais William Ruto muda wa kutekeleza mipango yake kwa nchi kabla ya kuhoji uwezo wake wa kuongoza.

Aidha walimtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Koome kukabiliana vikali na maandamano dhidi ya serikali. Pia walitishia kufichua majina ya watu wenye ushawishi waliodai wanafadhili maandamano ambayo yametangazwa kuwa haramu na Huduma ya Kitaifa ya Polisi.

 Odinga alizungumza jana Jumapili na kusema kwamba hawana mpango wa kusababisha machafuko katika nchi hiyo. Lakini wanapigania haki zao za msingi

“Tuna haki ya kuwaambia Wakenya ukweli kwa sababu Biblia inasema ukweli utawaweka huru. Tuna haki ya kuandamana kwa amani,” alisema Waziri Mkuu huyo wa zamani.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi