Connect with us

Kitaifa

LHRC yakosoa mabadiliko ya Toto Afya Kadi ya NHIF

Dar es Salaam. Siku moja tangu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kutangaza kusitisha utaratibu wa matumizi ya Toto Afya Kadi kwa watoto wakiwamo wanafunzi wa Shule ya msingi, Sekondari na elimu ya juu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimekosoa kikisema Sheria ya Mtoto imekiukwa.

Toto Afya Kadi ni kifurushi maalumu ambayo watoto walipatiwa huduma kwa mwaka mmoja kwa gharama ya Sh50, 400 lakini kutokana na maboresho mfumo huo umesitishwa.

Kupitia taarifa iliyotolewa kwa umma jana na kusainiwa na Meneja Uhusiano NHIF, Angela Mziray ilieleza kuwa mfuko huo unafanya maboresho ya usajilina huduma kwa watoto waliokuwa wanasajiliwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya ya ‘Toto Afya Kadi’.

“Hivyo katika kipindi hiki cha maboresho, wazazi wanashauriwa kusajili watoto wao kama wategemezi kupitia vifurushi vya Bima ya Afya au kupitia shule wanazosoma,”amendika kupitia taarifa hiyo.

Leo Machi 14, 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga amesema kituo hicho kimesikitishwa na uamuzi huo wa NHIF kwani ‘Toto Afya Kadi’ ni msaada mkubwa kwa watoto wengi wa Tanzania ambao hawana uwezo.

“Taarifa ya NHIF haijaweka bayana kuwa huduma hiyo imesitishwa kwa muda gani, uamuzi huu ni kinyume cha kifungu cha 8 cha Sheria ya Mtoto No 21 ya 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 ibara ya 24 ya mkataba wa Kimataifa wa Haki za mtoto 1989 na ibara ya 14 ya mkatana wa Afrika wa haki na ustawi wa mtoto 1989,” aliandika.

Amesema kusitishwa kwa huduma hiyo kunakwenda kuathiri watoto wengi kuutokana na ukweli kwamba idadi ndogo ya wazazi na walezi waliopo kwenye kwenye mfumo rasmi wa ajira.

“Ni Watanzania wacheche ndio wenye uwezo wa kumudu gharama za vifurushi ambavyo NHIF imependekeza wazazi wasajili,” amesema.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF leo akizungumza jijini Dodoma na Waandishi wa Habari amesema nia ya maboresho hayo  ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya wananchi wote kuwa na bima ya afya ambapo  watoto walio chini ya miaka 18  ni kundi kubwa ambalo kitakwimu ni zaidi ya nusu ya wnaanchi.

Amesema uafiti uliofanyika kuhusiana na ‘Toto Afya Kadi’ wanaamini wananchi wanaweza kulipia kupitia utaratibu waliouweka kwa sababu wapo watu wanaolipia.

“Leo hii kama ninaweza kununua bando la Sh2,000 kwa siku kwa ajili ya simu yangu na kupiga stori kwenye makundi kwa mwezi natumia Sh60,000 kwa mwaka natumia Sh720,000 sioni kwamba ni mzigo,” amesema

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi