Kitaifa
Polisi yawafungia kazi ‘panyarodi’, sita watiwa mbaroni Dar
Dar es Salaam. Zikiwa zimepita siku tano tangu kundi la vijana, maarufu ‘panya rodi’ kuvamia nyumba mtaa wa Idara ya Maji Bunju B jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi Kanda Maalum limewakamata watuhumiwa sita wakiwa na baadhi ya vitu zikiwemo simu na runinga.
Alisema lengo la operesheni hiyo ni kuhakikisha kila kitu kilichoibiwa kwenye matukio hayo vinapatikana, na kila aliyehusika kwenye tukio hilo anaingia kwenye msukosuko mkubwa wa kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani. “Wahalifu wanatafuta maeneo yenye udhaifu ndio wanafanya uhalifu, nitoe wito kwa wananchi kuacha fikra kuwa polisi atalinda kila mlango wa mwananchi, kuna mitazamo ya kusema hii kazi ni ya polisi, tufanye kama maeneo mengine falsafa ya ulinzi shirikishi,”alisema.
Mkazi wa Bunju Braightness Benjamin, alisema vijana hao walifika saa 7:20 akiwa amelala na mama yake na mtoto, wakaanza kusukuma mlango wakati huo dada yake akiwa sebuleni anajisomea.
Alisema alipoona hivyo na yeye akawa anausukuma kwa ndani huku akiita mwizi, walipofanikiwa kuingia wakamjeruhi mama yake huku wakiuliza zilipo simu.
“Walinifuata chumbani wakamchukua mtoto na kumning’iniza juu wakamuwekea panga wakisema kama nampenda niwape kila kitu ikiwemo fedha, simu na kompyuta mpakato, nikwaambia vile pale lakini hawakuridhika hadi wakapekua na kwenye pochi,”alisema.
Naye Eliamisa Urio, alisema kundi hilo la vijana baada ya kuvamia walichukua simu, fedha pamoja na kumjeruhi mume wake kwa kumkata kwa panga.
“Sikutegemea kama simu ingeweza kupatikana, Jeshi la Polisi limepambana,likimarisha ulinzi kiasi hiki uhalifu kama huu hauwezi kutokea tena,” alisema Urio.