Kitaifa
STARPECO: Lami baridi ni suluhisho la maendeleo ya miundombinu ya barabara nchini
![](https://chechetimes.com/wp-content/uploads/2024/12/ujenzi-pc.jpg)
Dar es Salaam. Miaka 18 iliyopita, ilizaliwa kampuni ya kwanza ya Kitanzania inayozalisha lami baridi (Bitumen Emul¬sion) ijulikanayo kwa jina la STARPE¬CO, wakati kama Taifa bado tunaendelea kutumia teknolojia ya lami joto ambayo utendaji wake ni wa kizamani na ghali.
Kutokana na sababu za ongezeko la watu, vyombo vya moto, mabadiliko ya tabianchi na uduni wa miundombinu ya barabara, ungeweza kutabiri kuwa barabara zetu zisingekuwa na maisha marefu kwa matumizi ya shughuli za kiu¬chumi na kijamii kutokana na uharibifu.
Azma ya kampuni hiyo ya kuchangia katika maendeleo ya miundombinu ya nchi ilidhihirika mwaka 2014, ambapo STARPECO ilizindua kiwanda cha lami baridi (Bitumen Emulsion) hapa nchini.
Malengo mahsusi ya uwekezaji huo, ni hatua ya kampuni hiyo kuitikia azimio la wadau wa barabara la mwaka 2014 kuwa juhudi za makusudi zifanyike na kila mdau (Serikali, taasisi za umma na binafsi, wataalamu nk.) nchi iwe katika ramani ya kutumia bidhaa za lami baridi kulingana na kasi ya dunia, nchi isiende¬lee kubaki nyuma katika teknolojia hii.
Akizungumza ofisini kwake, Mkuru¬genzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Gra-tian Nshekanabo amesema kuwa wao ni wasambaji au wazalishaji wa bidhaa za petroli (petro-chemicals) hususani vilainishi mitambo maalumu na vya kawaida na lami baridi (giligili) tangu mwaka 2014.
“Mwanzoni, tulianza na uzalishaji wa bidhaa za lami baridi za kugandisha mata¬baka ya lami yaani bidhaa inakaa katikati ya tabaka moja la lami na lingine – kitaal¬amu (Tackaot). Lakini baadaye, tukaanza kuzalisha lami baridi ya kuchanganyia na kufanya zege la lami (Cold mix asphalt (CMA) cement) ambayo moja ya manufaa yake ni ujenzi wa barabara mpya na pia kuwezesha ukarabati wa papo kwa papo kama vile kuziba viraka.”
Bidhaa zinazozalishwa na STARPECO
Akielezea bidhaa za lami zinazozal¬ishwa kiwandani hapo, amesema wana¬zo lami za kushikamanisha matabaka (Tackoat), kuchanganyizia kufanya zege la lami (CMA), bidhaa za kuimarisha eneo la barabara kabla ya kuweka lami ngu¬mu (Primer), au bidhaa za kuimarisha udongo (Soil Stabilization agents) zote zikiwa ni bidhaa muhimu katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha lami hapa nchini.
“Pia, sisi tumekuwa kampuni ya kwan¬za ya kizawa kuleta vilainishi mitambo vya hali ya juu. Tulianza na ELF, baadaye SWEPCO na sasa tunazo bidhaa mpya zinazodumu zaidi zitumikazo kwenye viwanda vya sukari, migodini na seh¬emu nyingine. Vilevile, tunayo bidhaa nyingine ya lami ngumu iitwayo Perfo¬mance Graded Bitumen (PGs) ambayo imesanifiwa na imependekezwa kutumi¬ka katika miradi mingi na hasa mipya inayotekelezwa sasa hapa nchini.”
Faida za kiuchumi na kimazingira za bidhaa za STARPECO
Nshekanabo amesema kuwa moja ya faida kubwa ya lami baridi ni urahisi wa kutumia bidhaa hizo, kazi kufanyika kwa haraka na kupunguza gharama.
“Mfano mfuko wa barabara unaeleke¬za kuwa viraka vya barabara vizibwe ndani ya saa 48 tangu vinapoonekana. Ni rahisi kutekeleza takwa hili kwa kutumia teknolojia ya lami baridi. Si rahisi kufa¬nya hivyo kwa teknolojia la lami joto. Ili ufanikishe hilo, kwa lami ya moto, una-hitaji uzalishe kiasi kikubwa cha zege la lami joto kama tani 10, za lami ili uwashe mtambo. Na ili kutumia kiasi hicho una¬bidi ukate viraka vingi mapema jambo ambalo linaongeza gharama na kutumia muda mrefu.
Hivi viraka vinapokaa muda mre¬fu bila kuzibwa vinaendelea kuharibu barabara, kingo zinaharibika na kutanu¬ka zaidi mwisho wake kuongeza eneo la kuziba. Kutengeneza viraka duni visivyodumu muda mrefu mbali kus¬ababisha adha kwa watumiaji ni hata ri kwa watumiaji wa barabara. Wakati ukiwa na lami baridi, unaweza ziba kiraka kimoja pekee. Unakata na kuziba hapo¬hapo na kikadumu sawa na maisha ya barabara nzima, Pia unaweza kufanya kazi katika mazingira ya mvua ndogo kitu ambacho hakiwezekani kwa lami joto.” amesema Mkurugenzi huyo.
Ameongeza kuwa lami ya baridi ina¬tumia muda mchache kukamilisha ujen¬zi kuliko ya moto ambayo itawahitaji wakandarasi kupumzika kila baada ya muda fulani kujipumzisha na ukali wa joto la lami pamoja na hewa chafu ya ukaa na hivyo kuchelewesha ukamilishaji wa zoezi la ujenzi.
Kwa jamii, teknolojia ya lami bari¬di inapotumika inawezesha barabara kukarabatiwa wakati wote na kutumika muda wote au matengenezo yanatumia muda mfupi hii hurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii za kila siku na hati¬maye kukuza kipato cha watumiaji wen¬gi wa barabara ikiwamo wasafirishaji, wasambazaji bidhaa, wachuuzi, wafany¬abiashara nk.
Amesema kuimarika kwa shughuli za kiuchumi kupitia miundombinu inayo¬tunzwa vizuri na lami baridi kunaakisi maendeleo ya huduma za kijamii (hos¬pitali, shule, benki, polisi na stendi) kwa kusaidia huduma hizo kufikiwa kwa ura¬hisi na muda wote kupitia vyombo vipi¬tavyo barabarani.
Katika faida za kimazingira, Nshekana¬bo amesema kuwa ujenzi na ukarabati wa barabara kwa kutumia lami za baridi ni rafiki wa mazingira kwa kuwa huepu¬sha; ukataji wa miti kwa ajili ya kuni au utumiaji mafuta kwa ajili za kuchemshia lami, uzalishaji wa hewa ukaa pamoja na ajali za moto wa vilipuzi kwa wakan¬darasi huku barabara ikibaki salama bila mashimo yanayoweza kusababisha ajali.
“Lami ya moto siyo nzuri kiafya, tafi¬ti zinaonesha kuwa baadhi wafanyaka¬zi wanaofanya kazi katika mazingira ya lami joto wako kwenye hatari ya kuathiri¬ka na magonjwa ya kansa au mifumo ya upumuaji. Mvuke wa lami ya moto ni hatari zaidi kwa binadamu na tabaka la ozoni,” ameongezea Mkurugenzi huyo.
STARPECO na mchango katika maende¬leo ya miundombinu
Nshekanabo amesema kuwa STARPE¬CO inachangia katika maendeleo ya miundombinu nchini kwa kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za lami baridi zenye ubora na gharama nafuu, ikilin¬ganishwa na siku za nyuma.
Amesema tangu waitikie wito wa Ser¬ikali wa uwekezaji katika lami baridi, na baadaye kiwanda cha uzalishaji kufun¬guliwa, wamekuwa wakishirikiana nao katika miradi mbalimbali ya miundom¬binu ikiwamo ule wa Mabasi yaendayo haraka (BRT).
Kuhusu uhamasishaji na elimu, Nshekanabo amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika kuan¬daa makongamano, semina, na mafunzo kuhusu lami baridi kwa mikoa mbalim¬bali hasa ikilenga wakala wa barabara na vyuo.
“Tumefanya mafunzo ya kuonge¬za ueledi na ujuzi wa lami baridi kwa wakala wa TANROADS zaidi ya mikoa kumi, TARURA mikoa tisa na ZANROADS huko Unguja na Pemba. Tumewatembe¬lea, tumefanya mafunzo ya nadharia na vitendo ya uzibaji viraka barabarani kwa njia baridi. Pia tumefanya tathmini ya utendaji wa hii techologia na bado zoezi ili linaendelea.
Mbali na jitihada hizo, STARPECO ime¬kuwa mjumbe katika kamati mbalimbali za kitaifa ikiwamo kamati ya Kitaalamu ya Barabara ( The Roads Technical Com¬mittee) ya Shirika la Viwango Tanzania – TBS, kamati ya viwango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ( The EAC Technical Committee, Civil and Building Engineer¬ing) huku ikijivunia rekodi ya kuwa kituo cha mafunzo kazini kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa zaidi ya miaka minane pamoja na kuwa kituo cha kufanyia utafiti kwa watafiti wa masuala ya lami.
“Tunazo barabara za mfano, tukizifa¬nyia tathmini kule Kigamboni, Morogoro na Dodoma. Mwaka 2019, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam usanifu wa lami baridi ( Cold Mix Asphalt- CMA) ulifanyika na baadaye barabara za mifano za Kileleni, Changanyikeni na Uvumbuzi, kwa ufadhili wa COSTECH, barabara zili¬jengwa/karabatiwa. Barabara zote zina¬fanya vizuri mpaka leo.
Mwaka uliofuata, kwa ufadhili wa Skills Development Fund, tulifanikiwa kuandaa barabara za mfano kule jijini Dodoma na kufundisha vijana zaidi ya 400 kwenye barabara ya Samia na Magufuli.”
Kwa upande wa sekta binafsi, amese¬ma kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiuza bidhaa zake nyingi kwa wakandarasi bin¬afsi nje na ndani ya nchi, wakubwa kwa wadogo, hiyo pekee inatosha kuonyesha namna gani sekta binafsi inajali bidhaa zao.
STARPECO imesambaza lami baridi kwa kujenga sakafu kwenye makazi bin¬afsi kama vile Goba, kwenye makanisa, hoteli za kitalii. Makampuni ya rangi ni watumiaji wa bidhaa zao kama malighafi.
Mafanikio
Amekiri kuwa wanajivunia kuwapo kwenye soko kwa miaka 18 ya uzalishaji bidhaa bora nchini na kubwa zaidi ni kuwa kampuni ya kwanza kuzalisha lami ya baridi na kusambaza vilainishi vya mitambo vya hali ya juu sana.
Hatua ya kuaminika kwenye kamati mbalimbali za Serikali na kikanda, kua¬minika kama kituo cha mafunzo na tafiti kwa wanafunzi na watafiti na ushiriki wao katika miradi ya Serikali ni jambo la kujivunia kwa kampuni hiyo ya kizawa.
“Tumeshiriki na kupata tuzo za TOP 100, tumeingia katika klabu ya CEort na kutambulika kama miongoni mwa makampuni makubwa, haya yote ni mafanikio kwetu na sasa kwa kiasi kikub¬wa neno lami baridi au giligili linaanza kujulikana katika jamii ya Watanzania.”
Changamoto
Licha ya faida zote za kiuchumi, kiu¬tendaji na kimazingira, Nshekanabo amekiri kuwa bado bidhaa ya lami bari¬di haifahamika wala kutumika ipasavyo, jambo linalochangiwa na kukosekana kwa mwongozo rasmi wa kitaifa kuhusu matumizi yake. Changamoto nyingine ni kasumba ya kukumbatia mazoea na jingine pia ni kasumba ya watu kutokua¬mini uwezo wa wazawa.
“Mtu au taasisi unamwelezea kitu na kinaonekana kuwa na manufaa mengi, lakini kwa kuwa anayewasilisha ni Mtan¬zania mzawa inakuwa ngumu kuamini sana tofauti na kinapokuwa kinawasilish¬wa na raia wa kigeni.”
Wito
Amewaomba wakandarasi, Serikali na wadau wa sekta ya miundombinu ya barabara kwa ujumla, kuanza kutumia lami baridi zenye faida nyingi kwenye maendeleo ya miundombinu ya barabara huku akitoa wito kwa Serikali kuharak¬isha mchakato wa kutoa mwongozo wa utumiaji wake.
![](http://chechetimes.com/wp-content/uploads/2023/02/chchelogo.png)