Connect with us

Kitaifa

Serikali yamwaga ajira za ualimu, nyingi za masomo ya amali

Dar es Salaam. Serikali imetangaza nafasi 3,633 za ajira za ualimu huku nyingi zikiwa za masomo ya amali.

Nafasi hizo zimetangazwa kupitia Sekretarieti ya Ajira jana Ijumaa Desemba 13, 2024, huku mwisho wa kutuma maombi ukiwa ni Desemba 20, 2024.

Kada hizo zinarandana na matakwa ya Sera ya Elimu ya mwaka 2013 toleo jipya la mwaka 2023, ambalo limetoa kipaumbele katika elimu ya amali kama mbinu mojawapo ya kukabiliana na tatizo la ajira kwa wahitimu.

Tangazo hilo limesema: “Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa,  anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi elfu tatu mia sita thelathini na tatu (3633) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.”

Tangazo hilo limesema walimu wanaohitajika ni wale wa masomo ya; biashara, ushonaji, uashi, umeme, ufundi magari, uchomeleaji na uundaji vyuma, sanaa, useremala, ufundi bomba, afya ya wanyama na uzalishaji chakula.

Wengine ni wa masomo ya kilimo na bustani, huduma ya chakula, upakaji rangi, umeme wa magari, jokofu na vipoza hewa, nishati ya jua, tehama, uvuvi, usindikaji mbao na mazoezi ya viungo.

Waombaji wametakiwa kutuma maombi yao katika tovuti ya ajira portal.

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi