Kitaifa
Milioni 400 kukabiliana mabadiliko ya tabianchi
TANGA : KUFUATIA changamoto ya athari ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye maeneo ya ukanda wa bahari ya Hindi Wilayani Mkinga serikali inatarajiwa kupeleka mradi wa shilingi milioni 400 Ili kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk.Ashatu Kijaji wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wanaoishi katika vijiji vinavyopakana na bahari ya Hindi Wilayani Mkinga
Amesema Wilaya ya Mkinga ni miongoni mwa wilaya ambazo zimeathiriwa na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi hivyo Ili kunusuru hali hiyo uwepo wa mradi huo utaweza kumaliza changamoto hiyo lakini na kutoa fursa ya ajira ya Kudumu kwa wananchi wanaoishi maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi
“Mradi huu unakwenda kudhibiti athari za mabadiliko ya tabia nchi ambayo tayari yameshaanza kuyaona katika maeneo yetu ya bahari Kwa kingo za ardhi kuanza kutafunwa na bahari”amesema Waziri Dkt Kijaji
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dk.Batlida Buriani amesema ushiriki wa wananchi katika kudhibiti uharibifu wa mazingira ikiwemo raslimali za bahari umesaidia zaidi ya wavuvi haramu 100 kusalimisha zana haramu kwenye vyombo vya Dola.