Connect with us

Kitaifa

Rais Samia kuanza kusikiliza kero za wananchi mmoja mmoja

Dar es Salaam. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi  (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametenga siku moja ya mwezi kuanza kusikiliza kero za mwananchi mmoja mmoja.

Amesema utaratibu huo utakuwa ukifanyika katika Ofisi ya Chama (CCM), Lumumba Dar es Salaam, Dodoma au Zanzibar kutokana na mahali atakapokuwa Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho tawala.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Machi 5, 2024 Makonda amesema Rais anafanya hivyo kwa kumuenzi Rais wa Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi aliyefariki hivi karibuni na kuzikwa Zanzibar.

Makonda amesema katika kumuenzi Rais Mwinyi aliyekuwa na utaratibu huo, Samia ataanza kusikiliza kero za mwananchi mmoja mmoja mara moja kwa mwezi.

 “Mwananchi atakayekuja kuleta kero yake kwa Rais na kuwa kwenye ratiba atalazimika kuwa na taarifa kuwa jambo lake halikupatiwa majibu chini.

“Atamsikiliza yeyote bila kujali elimu wala rangi, ndio tumetangaza, hivyo utaratibu utapangwa na wananchi watatangaziwa,” amesema Makonda alipoulizwa kuhusu utaratibu wa jambo hilo.

Amesema, Rais anafanya hivyo kwa sababu kubwa tatu.

“Kwanza ni kudumisha na kudhihirisha kwa vitendo viongozi kuwasikiliza wananchi, pili ni kumuenzi Rais Mwinyi aliyekuwa na utaratibu huo na kwa mujibu wa Ilani ya chama na Katiba inayosema tumia cheo chako kwa manufaa ya wengine.”

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi