Connect with us

Kitaifa

Mvua yatikisa Morogoro, wananchi wavushwa kwa kamba

Mmoja wa wananchi waliokutwa wakivushwa, Shani Ally amesema kwa muda mrefu eneo hilo limekuwa korofi  na kwamba kwa mvua za mwaka huu hali imekuwa mbaya zaidi.

“Mvua ya jana ilianza saa 11 jioni na haijakatija mpaka muda huu saa 3 asubuhi, nimelazimika kumpeleka mtoto wangu shule kwa kuwa hakuna gari inayopita hapa,” amesema Shani.

Diwani wa Lukobe, Selestine Mbilinyi amesema mvua za mwaka huu zimeleta madhara makubwa kuliko zilizotokea miaka ya nyuma.

“Watu wamepoteza maisha, makazi, mali na hata miundombinu nayo imeharibika kwa kiasi kikubwa,” amesema na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu huku akiwasisitiza kuchukua tahadhari, ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Ameishukuru Serikali ya Wilaya na Mkoa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa hatua za haraka zilizochukuliwa ambazo zimepunguza madhara.

Maeneo mengine yaliyoathirika na mvua hiyo katika Manispaa ya Morogoro ni pamoja na Mkundi, Lugala, Kasanga, Bigwa, Mafisa na Mwembesongo.

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi