Connect with us

Kitaifa

Tanzania yaongoza duniani kupeleka maji vijijini

Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dk Victoria Kwakwa ameitaja na ameipongeza Tanzania kuwa kinara na mfano katika utekelezaji wa programu ya uendelevu wa huduma ya maji na usafi wa mazingira vijijini, Mashariki na Kusini mwa Afrika na Duniani kwa kutumumia utaratibu wa malipo kwa matokeo yaani Programme for Results (PforR) ambayo inatekelezwa katika nchi zaidi ya 50 na kufadhiliwa na Benki ya Dunia.

 Akizungumza na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba pamoja na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Makamu wa Rais Kwakwa amesema Tanzania ni mfano bora katika utekelezaji wa Programu ya PforR na ameiomba itoe uzoefu wa mafanikio yake kwa nchi zaidi ya 23 kutoka kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika zinazoshiriki mkutano wa maji na usafi wa mazingira (WASH Leadership Summit).

Awali, Tanzania ilipata Dola za Kimarekani milioni 350 katika miaka mitano lakini ndani ya miaka mitatu ya kwanza ilikuwa imefikisha maji kwa zaidi ya watu wapya milioni 4.7 vijijini katika mikoa 17.

Kufuatia mafanikio hayo, kulingana na matokeo hayo, Benki ya Dunia imeiongezea Tanzania Dola za Marekani milioni 300 na hivyo kupanua wigo wa utekelezaji kufikia mikoa 25. Kwa sasa Sh970 milioni zimepelekwa katika kila halmashauri kwa ajili ya kuanza utekelezaji.

Aidha, mafanikio haya yamefungua rasmi milango ya uendelevu wa programu hii ambayo inafikia ukomo Julai 2025. Kufuatia hoja ya Tanzania ya kuwa na PforR Awamu ya Pili, Benki ya Dunia imeonesha utayari wa kuwa na PforR Awamu ya Pili katika kipindi cha 2025-2030.

Wizara ya Maji kupitia programu hii ya lipa kwa matokeo (PforR) imetekeleza zaidi ya miradi ya maji 1,500 ambayo imekamilika na inatoa huduma.

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi