Siasa

Nyongo ya Martin Maranja: Slaa haipendi CHADEMA

Slaa ametumia mdomo wake, mkono wake na uwezo wake wote kuondoa uhalali wa kisiasa wa CHADEMA katika jamii tangu alipoondoka CHADEMA. Amesema na kuandika mabaya dhidi ya CHADEMA. Slaa anachukizwa na lolote linalofanywa na CHADEMA.

Leo anatafuta jukwaa la kisiasa kufanya udalali wake siyo kwamba anataka kurejea CHADEMA. Slaa awamu ya tano yote alitetea dhuluma ya uchaguzi wa 2020 na matokeo yake. Baada ya kustaafu ubalozi anatarajia katika awamu ya sita avune matunda ya haki? Haiwezekani. Utavuna ulichopanda.

Kuna kitu muhimu sana Slaa na waunga juhudi wengine wanaruka. Lazima wasaliti, waunga juhudi wakitaka kurejea CHADEMA wakiri dhambi zao, wajutie makosa yao ya usaliti na wasamehewe. Hakuna msamaha bila toba. Hatujasahau hata kidogo biashara yao haramu. Tupo makini sana wakati huu.

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi