Connect with us

Kitaifa

Tetesi: Lissu arejea Ubelgiji kwa muda kwa matibabu ya msongo wa mawazo

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amerejea nchini Ubelgiji kwa matibabu ya msongo wa mawazo. Chanzo cha taarifa kinasema, Lissu anatibiwa katika hospitali ya UZ Leuven (pichani). Hospitali hiyo mali ya Kanisa Katoliki Ubelgiji ni moja ya hospitali maarufu zaidi nchini humo na ndipo alipotibiwa Lissu baada ya shambulio dhidi ya uhai wake mwaka 2017 jijini Dodoma. Umoja wa Watanzania nchini Ubelgiji na uongozi wa CHADEMA wamethibitisha safari ya Lissu.

Japo amepona majeraha ya shambulio la risasi, Lissu hivi sasa anatajwa kuwa na tatizo la afya ya akili linalojulikana kama Posttraumatic Stress Disorder (PTSD). Tatizo hilo huwakumbuka baadhi ya watu baada ya kupitia matukio makubwa ya kutishia uhai. Mtandao wa magonjwa ya akili wa psychiatry dot org unataja yafuatayo kuwa dalali za maradhi hayo ya akili:

1. Kuota ndoto mbaya mara kwa mara hasa zinazohusiano na tishio la uhai na kifo.
2. Kutotokea kwenye miadi bila taarifa muda akili inapojaribu kujiepusha na watu.
3. Ulevi wa aina mbalimbali katika kujaribu kuondoa mawazo mabaya.
4. Mawazo hasi kuhusu maisha, wasiwasi na kupoteza imani ya kupata furaha kwenye maisha.
5. Hasira wakati mwingine zinazopitiliza na kushindwa kupatana/kusuluhisha kirahisi.

PTSD ni moja ya magonjwa korofi ya akili katika zama za hivi karibuni. Wataalamu wa magonjwa ya akili wanasema ugonjwa huu unatibika iwapo mgonjwa atapata tiba sahihi na kwa wakati. Inatia faraja kwamba Lissu ameanza matibabu haya na anayapata kutoka hospitali bingwa duniani. Taarifa zinasema atakuwa anapata matibabu katika vipindi mbalimbali huku akiwa anarejea nchini na kuendelea na shughuli zake kama kawaida wakati anatumia dawa na ushauri wa madaktari. Bila afya njema ya akili hakuna maisha.

Inatia huzuni kuona mtu kwa mfano akisimama jukwaani kuhutubia mchana, kisha usiku inambidi kutumia kilevi kikubwa ili kupata usingizi jambo ambalo linazidi kuathiri ufanisi wa akili na utendaji. Jukumu la kila mmoja wetu ni kuendelea kumuombea kupona na kuendelea na maisha kama awali.

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi