Connect with us

Kitaifa

Baraza la Vyama vya Siasa latoa ‘dukuduku’ mbele ya Rais

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Juma Ali Khatibu amesema siyo tu vyama vya siasa vilizuiliwa kufanya mikutano ya hadhara katika kipindi cha miaka sita iliyopita bali hata baraza hilo lilikuwa halikutani.

Khatibu ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 11, 2023 wakati wa mkutano maalumu wa baraza la vyama vya siasa na wadau wa demokrasia unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo amesema mkutano huo ni maalumu uliotokana na agizo alilolitoa Rais Samia Suluhu Hassan kwa msajili wa vyama vya siasa kuitisha mkutano wa wadau kujadili masuala ya demokrasia.

Amesema msajili wa vyama vya siasa alikaa na baraza la vyama vya siasa na kamati ya uongozi ya baraza la vyama vya siasa na kufanikisha mkutano huo.

“Baraza la vyama vya siasa linakupongeza kwa kazi kubwa unayofanya ya kuimarisha demokrasia na kutunza amani ya nchi. Tunakushukuru kwa kufungua na kutoa ruhusa ya kufanyika kwa mikutano ya hadhara. Kabla ya yeye kuwa Rais vyama vya siasa nchini havikuwa na fursa hiyo kwa miaka sita iliyopita.

“Hata baraza la vyama vya siasa lilikuwa halikutani, mwenyekiti aliyenitangulia alikaa kwa miaka minne lakini baraza lilikuwa halikutani kwa hiyo uwepo wako umewezesha baraza lifanye kazi na mkutano huu tumeuona,” amesema Khatibu.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi