Biashara
Nyaraka za siri .. familia mbili zilivyoifisadi bandari ya Dar kwa zaidi ya miaka 20
Nyaraka za siri zinazoonesha jinsi familia mbili za Tanzania zilivyosuka mipango ya kuinyonya bandari ya Dar kwa zaidi ya miaka 22 kupitia kampuni ya TICTS na makampuni mengine tanzu kama inavyoonekana zimevuja mtandaoni…. Familia hizo zinaongozwa na Nazir Karamagi (Waziri wa zamani mwenye kashfa ya kusaini mkataba wa serikali hotelini Jijini London) na Yogesh Manek (mmiliki wa Benki ya Exim Tanzania). Wote Karamagi na Manek wanatajwa pia kuwa na pasi za kusafiria zaidi ya ile ya Tanzania jambo ambalo ni kinyume na sheria kwani Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili.
Septemba 2017 aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati John Magufuli alianza mchakato wa kuing’oa TICTS kutoka bandari ya Dar kwa kuwanyima mkataba wa muda mrefu. Mwisho wa mwaka jana Rais Samia Suluhu akaendeleza mchakato huo na kampuni gwiji la mambo ya bandari duniani DP World kupewa nafasi ya kushirikiana na Tanzania kuboresha bandari. Hata hivyo familia hizo mbili zimeendelea kutumia mabilioni ya shilingi zikihonga wanaharakati na wanaharakati kupinga na kupotosha kuhusu zoezi hilo la mabadiliko yenye tija bandarini. Hizi hapa nyaraka za umiliki na janja janja ya walivyosuka kuizunguka serikali kwa zaidi ya miaka 22.
Chanzo chetu kinasema kuwa Rais Samia amekusudia kufutilia mbali kundi hilo na mapema jana Nazir Karamagi alionekana kwenye mkutano wa CCM akijaribu kujisafisha.