Connect with us

Kitaifa

Serikali yafafanua utoaji mikopo vyuo vya kati

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amewatoa hofu Watanzania kuhusu utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo binafsi na vya kati na kutoa ufafanuzi wa utoaji wa mikopo hiyo kwa vyuo vya kati.

Dk Mwigulu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Juni 26, 2023 wakati akihitimisha hoja mjadala wa hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali.

Waziri amesema kumekuwa na kelele za hofu kuhusu mikopo kutolewa kwa vyuo vya kati ambavyo ni vya Serikali pekee.

“Ni kweli kwamba, tumeanza na waliopangwa vyuo vya kati vya Serikali, waheshimiwa wabunge mtambue kuwa hata kwa vyuo vya juu tulianza na vile vya Serikali ndipo tukaja kwenye taasisi kwa bajeti ya mwakani tutaingia huko,” amesema Dk Mwigulu.

Dk Mwigulu ameeleza kuwa Serikali ina nia ya kusaidia vijana wa Kitanzania kupata elimu hasa wale wanaotoka kwenye familia maskini.

Akizungumzia mikopo kwa wanafunzi, amesema kwa mwaka huu Serikali imetenga Sh700 bilioni kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo vya juu lakini itapanda hadi Sh800 bilioni watakapoanza kutoa mikopo kwa vyuo vya kati.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi