Kitaifa
Tuhuma: Mbunge Ole Sendeka alipwa mamilioni kutetea ufisadi bandarini
Kuna taarifa zinaenea kwamba Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole-Sendeka amelipwa mamilioni ya shilingi kupinga fagio la kusafisha ufisadi kwenye bandari ya Dar es Salaam.
Kwa zaidi ya miaka 20 kampuni ya kuhudumia makontena TICTS imekuwa ikisuasua kwenye kutoa huduma bandarini. Alipoingia Rais Magufuli akajiapiza kuifuta na akaipa muda kujiandaa kuondoka. Bahati mbaya akafa kabla ya utekelezaji. Alipoingia Samia akatekeleza kwa kuiondoa kabisa bandarini.
Hata hivyo inasemekana wamiliki wa TICTS ambao ni Nazir Karamagi na Yogesh Manek wameanza kulipa mamilioni kwa baadhi ya Wabunge ili kupinga hatua hiyo ya serikali. Mmoja ya wabunge hao ni Christopher Ole Sendeka. Sendeka ana kashfa nyingi ikiwemo ufisadi na kugushi vyeti vya elimu yake. Kwa kumbukumbu tu, Karamagi akiwa Waziri aliwahi kusaini mkataba wa madini London akiwa hotelini na wazungu).
Siku za karibuni kumekuwa na magenge ya kihalifu kujaribu kuzuia mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji wa bandari na mamlaka ya mapato. Maganga haya ni yale ya wafanyabiashara ambao walikuwa wakinufaika na mifumo hiyo kwa zaidi ya miaka 20.
Je Samia atawezana na magenge haya? Iwapo atapata msaada wa kutosha wa vyombo ya ulinzi na usalama ana nafasi kubwa ya kumaliza magenge haya.