Kitaifa
Kampuni ya mafuta na gesi Tanzania yatangaza kufilisika
Kampuni kubwa ya mafuta na gesi ya Tanzania, Swala Tanzania Plc, imetoa tangazao ya kwamba imeanza mchakato wa kuuza mali zake kutokana na ukata mkubwa wa kifedha unayoikumba kampuni hiyo ya kwanza nchi ya mafuta ya gesi, kusajiliwa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
Baada ya kikao cha bodi ya wanahisa, ambao wanawakilisha takriban 75% ya wanahisa wake, mkutano wa tarehe 31 Machi 2023 uliamua kuwa kampuni hiyo ya mafuta na gesi ianze mchakato wa kufilisiwa kwa kuuzwa mali zake kutokana na kushindwa kujiendesha.
Kampuni ya mafuta ya gesi ya Swala ni kampuni yenye makao makuu Dar es Salaam, Tanzania, na leseni ya kuchimba mafuta na gesi ndani ya mfumo wa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Pia inalimiki leseni utafiti ya ufiti wa kitalu cha Kilosa-Kilombero na uwekezaji katika PanAfrican Energy Corporation (PAE), yenye takriban km² 17,300 ya eneo la ardhi ambapo Kampuni hiyo iliundwa mnamo Julai 2011.
Historia ya kuanguka kwa Kampuni ya Mafuta ya Gesi ya Swala inarudi nyuma hadi mwaka 2017, wakati kampuni hiyo, kupitia kampuni yake tanzu inayoimiliki kikamilifu, Swala (PAEM), ilikubaliana na Orca Energy Corporation (OCRA) kununua asilimia 7.933 ya hisa katika PanAfrican Energy Corporation (PAEC). Hatimaye, mkataba huo ulikwenda vibaya baada ya kampuni tano kubwa za nishati zilizohusika katika mchakato mzima wa biashara katika mkataba huo kutozwa faini kubwa na Tume ya Ushindani (FCC) kwa kufunga ununuzi bila taarifa rasmi kwa FCC.
Faini zilizotozwa kwa kampuni ni pamoja na Swala PanAfrican Energy Mining ($177,712.20), Orca Exploration Group Inc ($2,888,300), PAE Pan African Energy Corporation ($2,888,300), Swala Oil and Gas Tanzania ($137,716) na PanAfrican Energy Tanzania Limited ($2,888,300).
Kulingana na mkataba huo ambalo ulikuwa na makosa kisheria hadi kupewa adhabu na Tume ya Ushindani, Swala Tanzania iliingia makubaliano iwe na hisa 7.9% za ORCA Exploration Group Inc katika PAE PanAfrican Energy Corporation (PAEM) kupitia Swala UK, tanzu inayomilikiwa kikamilifu na Swala Tanzania.
Hivyo basi, kulingana na barua ya kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala iliyotolewa tarehe 3 Aprili 2023, ambayo inatangaza kuanza kwa mchakato wa uuzaji wa kampuni, kampuni hiyo inasadiki kwamba PAEC inamiliki asilimia 100 ya PanAfrica Energy Tanzania Limited na pia ndiyo mmiliki pekee wa Kitalu cha gesi cha Songo Songo, kampuni tajwa inapinga madai ya kodi nchini Tanzania yenye jumla ya USD milioni 55 (kufikia tarehe 31 Desemba 2022), ambayo baadhi yake ni ya tangu mwaka 2008. Hata hivyo, licha ya maombi ya kufanya hivyo, ORCA haijatoa sababu za kibiashara kwa Swala (PAEM) juu ya changamoto zilizopo.
Kulingana na barua iliyotoka, inaonekana kwamba ORCA, kupitia umiliki wake wa PAET, imehusika katika utovu wa nidhamu na uvunjaji wa Mkataba wa Wanahisa na majukumu yake chini ya sheria ya Mauritius, nchi iliposajiliwa; ORCA inatuhumiwa kwa ubadhirifu na utapeli wa fedha na mali zinazomilikiwa na PAET ili kulipia gharama zake, na PAEC, ambayo iko chini ya umiliki wa ORCA, haikuchukua hatua kushughulikia suala hili.
Kushindwa kwa ORCA kutoa akaunti zinazolingana na viwango vya IFRS imeizuia Swala kupata taarifa muhimu za matumizi ya fedha ambazo kimsingi zingeweza kuisaidia kubaini kiwango cha uvunjaji wa mkataba na kuchukua hatua za haraka kuinusu kampuni. Zaidi ya hayo, ORCA imefaidika kinyume na sheria za mkataba na kuigubika kampuni ya Swala matatizo, kwa kutumia fedha ambazo kimsingi zingetengwa kwa ajili ya Swala kutatua changamoto zake za kodi nchini Tanzania.
Hatua hizi zinaweza kuchukuliwa kuwa ni uvunjaji wa uaminifu na ukiukwaji wa mkataba kati ya ORCA na PAEC. Kwa mfano, Swala (PAEM) hivi imeshindwa kabisa kupata fedha ambazo zingetakiwa kuisaidia kampuni hiyo kutatua changamoyo zake za kifedha kulingana na makubaliano ya uwekezaji na wanahisa. Hii inamaanisha kwamba Swala yenyewe haina fedha za kutosha, hivyo kupelekea wanahisa kuamua kwamba Swala ifilisiwe. Kimsingi, hatua za ORCA zilisababisha madhara ya kifedha kwa Swala na kusababisha hali yake ya kutokumudu madeni.
Kampuni ya Swala Tanzania Plc ikiwa kampuni ya kwanza ya mafuta na gesi iliyoorodheshwa kwenye soko la hisa itaathiri karibu wanahisa 2000 wa ndani.
Apex Corporate Trustees (UK) Limited, ambayo inawajibika kwa kusimamia usalama kwa niaba ya Conover Investments LP, ilinunua Noti za Juu (Senior Notes) ambazo Swala (PAEM) ilitoa mwezi Desemba 2017 kununua hisa katika PAEC. Sasa wameteua wasimamizi kwa Swala (PAEM) Limited kulingana na haki zao chini ya makubaliano ya usalama.
Kulingana na masharti ya Mkataba wa Uzalishaji wa Sehemu (Production Sharing Agreement) ambao Swala ilisaini na TPDC na Serikali ya Tanzania, umiliki wa leseni ya Kilosa-Kilombero utarejeshwa kwa TPDC.
Bwana Welwel atakuwa na jukumu la kushughulikia mchakato wa kufuta kampuni. Atafanya kazi na wadai na wanahisa wa kampuni kwa wakati unaofaa.