Connect with us

Kimataifa

Maelfu wavamia shamba la Kenyatta waiba mifugo

Kenya. Kundi la watu wanaokadiriwa kufika zaidi ya 1,000 wamevamia shamba la Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta mapema leo Jumatatu Machi 27, 2023 hii, huku ikishuhudiwa mwendelezo wa maandamano ya upinzani yaliyoitishwa kila Jumatatu.

Watu hao wameonekana, wakikata miti kwa kutumia misumeno ya umeme (Chain Saw), kuiba mifugo kwa idadi isiyojulikana kisha kuchoma moto sehemu ya shamba hilo lililopo Kaunti ndogo ya Ruiru.

Tovuti ya The Standard ya nchini humo imeripoti kuwa kundi hilo linadaiwa kuwatishia kuwakata mapanga waandishi wa habari na watu watakaothubutu kuwarekodi kinachoendelea shambani hapo.

Aidha katika video za siri zilizovuja kwenye mtandao wa Twitter zimewaonyesha wavamizi wakiondoka na mifugo ikiwemo mbuzi na kondoo, Taarifa zinasema bado sababu ya uvamizi huo haijajulikana.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi