Connect with us

Makala

Wafahamu wana CCM 9 wanaotajwa kusuka mipango kushindana na Rais Samia 2025

Machi 19 mwaka 2021 Rais Samia aliingia madarakani kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kifo cha Rais John Magufuli. Habari za ndani zinaelea kuingia kwake madarakani japo ilikuwa ni takwa la Katiba kulijaribu kuwekewa uzibe na baadhi ya makundi ya wahafadhina ndani ya CCM, ndani ya Serikali na hata nje. Rais Samia anawafahamu watu hao na inaelekea anatumia sayansi ya hali ya juu kudili nao mmoja baada ya mwingine tangu aingie madarakani. 

Utafiti wa Cheche Times kupitia vyanzo vyake mbalimbali ndani na nje ya CCM unaonesha Samia hatakuwa na upinzani mkubwa nje ya CCM mwaka 2025 ambapo wapinzani wengi hasa watakiwa wakijaribu kwanza kurejea Bungeni (Lissu, Mbowe, na kadhalika). Hata hivyo upinzani unatarajiwa ndani ya CCM na baadhi ya majina na makundi yanatajwa. 

Kundi la kwanza linatajwa kuwa kundi la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambalo wachambuzi wanasema licha ya kwamba Majaliwa mwenyewe inawezekana anaogopa kujaribu jambo hilo kwani anajua matokeo yake wako watu wanamtumia. Kundi hilo lina waratibu wakubwa wawili ambao ni Mbunge wa Mbarali mkoani Mbeya, Haroon Pirmohamed na Mfanyabiashara wa Dar es Salaam Bwana Salim Abdallah Muhene. Hawa wawili wamekuwa vinara wa kundi hili. Kiungo chao ni mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa Bwana Saad Majaliwa ambaye pia wanampa miongozo na mbinu za kibiashara. Kwenye kundi hili pia anatajwa Spika aliyevuliwa wadhifa wake Job Ndugai. 

Ndugai na Haroon Pirmohamed

Kundi la pili ni kundi la Mbunge Luhaga Mpina. Kundi hili lina viongozi wake nyuma ya pazia na Mpina anaonekana kama anatumwa tu. Wanaotajwa kuwa ndani ya kundi hili ni Humphrey Polepole, Leonard Chamuriho na Medard Kalemani. Hata hivyo Luhaga bado anapambana na kashfa ya kuuza ranchi za serikali na ile ya kuchoma moto nyavu za wavuvi jambo ambalo liliwarudisha maelfu ya wavuvi katika umaskini mkubwa. 

Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina

Kwenye siasa siku moja ni muda mrefu sana. Bado tuna karibu miaka miwili  kufikia Uchaguzi Mkuu 2025, iwapo makundi hayo yatafanikiwa kumtikisa Rais Samia au la ni swala la kusubiri kuona. 

 

Ndimi Luqman Murilo

Safarini Mitwero Lindi

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi