Connect with us

Kitaifa

Kampuni ya GSM yashutumiwa kwa ufisadi na ukwepaji kodi bandarini

Taarifa hii imefika Cheche Times toka kwa mtu aliyejitambulisha kama mfanyakazi wa TRA Dar es salaam na kwa sababu za kuhofia usalama wake ameomba asitajwe jina.

“Mheshimiwa Rais, kuna genge la uharamia ambao ulikuwepo tawala za nyuma kwenye eneo la ukwepaji kodi pale bandari ya Dar na TRA. Genge hili lilinufaika sana wakati wa utawala wa Kikwete baadaye likajaribu na kuzimwa kwa kiasi kikubwa wakati wa Magufuli.
Genge hili kwa kiasi kikubwa linaisaidia kampuni ya GSM kukwepa kodi na uharamia mwingi kwenye bandari yetu. Mamia ya kontena zinaingizwa siku hizi bila kulipiwa kodi stahiki na badala yake wanapewa kadirio la kodi ndogo na kuinyima nchi mapato.

Vyombo vya ulinzi na usalama mko wapi kumsaidia Rais kuondoa ufisadi huu wa GSM bandarini na TRA? Kampuni hii inashirikiana na maafisa wa serikali kwenye maeneo hayo. Msaidieni Rais, kawapa nafasi na mamlaka mfanye kazi basi ifanyeni kwa weledi. Imefikia mahali wakurugenzi wa GSM akiwepo Ghalib wanasema TRA na Bandari wanazo mfukoni. Hii ni aibu.”

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi