Connect with us

Kitaifa

Google mbioni kuondoa ‘password’ katika programu zake

Marekani. Kampuni ya Google imesema ipo mbioni kuachana na matumizi ya nywila (password) katika ulinzi wa programu zake katika vifaa rununu ikiwamo kwenye mifumo yake huku ikiitaja njia hiyo kuwa ni ya kizamani na ngumu.

Kwa mujibu wa CNN imeripoti kuwa kampuni hiyo imesema badala ya kutumia nywila katika ulinzi, wateja wao watashauriwa kutumia alama za vidole na utambulisho wa sura,

Hayo yamesemwa jana Jumapili Oktoba 15, 2023 katika tovuti ya Google huku ikisema mfumo huo mpya hautakuwa na haja ya mtumiaji wao kukariri nywila zake.

“Tutaendelea kuhimiza tasnia na wateja wetu kuacha kutumia nywila katika ulinzi wa program zao na badala yake watumie njia mpya kama mbadala, huku nywila tukiendelea kuziondoa taratibu na baadaye kuzifuta kabisa,” Google iliandika.

Wakati Google ikitangaza hatua hiyo tayari programu za YouTube, Uber na eBay zimeanza kuachana na matumizi ya nywila na badala yake matumizi ya utambulisho wa sura na alama za vidole yakitumika zaidi.

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi