Kimataifa
Balozi wa Marekani: Demokrasia Tanzania izingatie mazingira ya nchi
BALOZI wa Marekani nchini Tanzania, Michael A. Battle, amesema demokrasia ya nchi inapaswa kuendana na mazingira yake mahususi badala ya kutegemea kufanana duniani.
Akizungumza katika Mkutano wa Demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Balozi Battle amasema kwa mfano demokrasia ya Tanzania haiwezi kufanana na demokrasia ya nchi za kifalme [kama Uingereza] na sio lazima ifafane na mifumo mingine ya kiutawala inayotumiwa na nchi nyingine duniani.
“Demokrasa ya Tanzania ni lazima izingatie muktadha na mazingira ya Tanzania, na iakisi matakwa ya watazania wenyewe. Nchi yotote duniani haina haki ya kuipangia Tanzania aina ya mfumo wake wa demokrasia,” alisema Balozi Battle.
Aidha, Balozi Battle amesema Marekani inajivunia sana hatua kubwa alizochukua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuboresha demokrasia nchini Tanzania.