Connect with us

Makala

Hizi hapa fani zenye mshahara mnene

Uchambuzi wa Data (Data Analysis)

Taaluma ya kwanza inayolipa zaidi kulingana na utafiti wa tovuti mbalimbali ikiwemo Smooth remort ni, Uchambuzi wa data, ambao kimsingi unahitajika katika tasnia mbalimbali ikiwemo afya, fedha, elimu pamoja na habari.

Kadiri taasisi na biashara zinavyozidi kutegemea ufanyaji maamuzi unaoendeshwa na data, zinahitaji wafanyakazi zaidi wenye uwezo wa kukusanya, kutafsiri na kushiriki data ambayo inaweza kutatua matatizo yao ya biashara wataalamu hao hutafutwa mno.

Uchanganuzi wa data ni mchakato wa kuleta maana ya seti kubwa za data ili kupata maarifa na kufahamisha uchanganuzi wa biashara na kufanya maamuzi yanayohusiana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Afrika, Nuzulack Dausen anasema ndani ya miaka hii mitano uchambuzi wa data umeongezeka thamani sio tu Tanzania hata duniani kutokana kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa wachambuzi.

Anasema kama kuna mtu anataka kuwa bobezi katika eneo hilo, anapaswa kusoma masomo ya takwimu.

‘’Pia anaweza kusoma masomo ya uchambuzi wa data ‘data analyst’ inayopatikana hata mtandaoni,’’ anasema Dausen ambaye naye ni mmoja wa wasomi waliojikita katika uandishi wa uchambuzi wa takwimu sambamba na kutoa ujuzi huo kwa wengine. Anasema kwa sasa taaisisi mbalimbali kama benki zinahitaji wataalamu wa fani hiyo,

Wanasayansi wa data hupata wastani wa mshahara wa dola za kimarekani 82,360 sawa na Sh200, 948,599 kwa mwaka kulingana na Ofisi ya Marekani ya Takwimu za Kazi.

Kwa Tanzania kwa mujibu wa Grassdoor makadirio ya jumla ya malipo ya mchambuzi wa data ni Sh4,950,000 kwa mwezi.

Watu wenye ujuzi katika uchanganuzi wa data wanaweza kutumia zana mbalimbali ikiwa ni pamoja na Microsoft Excel, majedwali ya Google, SQL, Tableau, R, au Python.

Kwa kawaida wachanganuzi wa data hutumia mbinu za hisabati na uchanganuzi kubadilisha data kuwa maamuzi bora ya biashara yanayoendeshwa na data.

Kadiri idadi ya data inayopatikana kwa biashara inavyoongezeka, ndivyo pia mahitaji ya wachanganuzi wa data wenye ujuzi kuichakata na kuitafsiri wanavyohitajika Wachambuzi wa data kwa kawaida hulipwa vizuri kwa ujuzi wao.

Usalama wa Mtandao (Cyber Security)

Taaluma ya usalama wa mtandao inahusika na ulinzi dhidi ya vitisho vya mtandao. Mashambulizi ya mtandao yameawaachia maumivu watu wengi duniani. Na sio watu binafsi kudukuliwa tu taarifa zao, lakini hata taasisi, kampuni na mashirika hayajasalimika.

Wataalamu wa usalama wa mtandao wanahitajika ili kutambua, kudhibiti na kupunguza hatarim ya mashambulizi haya, hivyo kuonekana kuwa lulu hasa kwa uchache wao.

Mtaalamu wa mifumo ya kompyuta, William Sunguya anasema kadiri muda unavyoenda taaluma hii inazidi kupanda thamani kutokana na teknolojia kukua karibu kila sehemu ya maisha ya sasa.

Sunguya anasema kutokana na kukua kwa teknolojia katika mtandao, hata wadukuzi nao wanazidi kuongezeka, ndio maana kampuni na taasisi zinaajiri walinzi wa mtandao.

‘’Mtu anayetaka kuwa mlinzi wa mtandao anapaswa asome masomo ya sayansi na akifika chuo asome Information technology (IT) kisha abobee kwenye usalama wa mtandao,’’ anaeleza.

Sunguya anasema watu wanaobobea huko wanapaswa wajue maendeleo ya mtandao kutokana na mtandao kuboreshwa kila siku.

Taaluma hii kiwango chake cha juu cha malipo kwa mwezi nchini Tanzania ni Sh2,770,041 ambapo kwa mwaka ni Sh33,240,500 hii ni kwa mujibu wa tovuti ya World Salary.

Usimamizi wa Miradi (Project Management)

Usimamizi wa mradi ni ujuzi unaohusika na kupanga na kutekeleza miradi, ikiwemo kukidhi bajeti.

Usimamizi wa mradi hutoa muundo na udhibiti wa mazingira ya mradi ili shughuli zilizokubaliwa zitoe huduma zinazofaa kukidhi matarajio ya mteja. Miradi ni miundo ya muda ambayo lazima isimamiwe na kudhibitiwa ipasavyo ili kukidhi malengo yaliyowekwa.

Kulingana na tovuti mbalimbali zikiwemo marketsplash na courser, Usimamizi wa miradi ni taaluma muhimu inayohusiha matumizi ya maarifa maalum, ujuzi, zana na mbinu ili kutoa kitu cha thamani kwa watu.

Miradi kama biashara, ujenzi wa majengo, juhudi za kutoa msaada baada ya janga la asili, upanuzi wa mauzo sokoni ni mifano ya mradi inayohitaji usimamizi ambayo unahusisha kupanga, kudhibiti, na kusambaza rasilimali ili kufikia malengo na malengo mahususi.

Wasimamizi wa mradi huhakikisha kuwa mambo yanafanyika kwa wakati, na majukumu yao ni pamoja na kuweka malengo na tarehe za mwisho, kuratibu na kufuatilia washiriki wa timu ili kuhakikisha wanafikia malengo hayo.

Kulingana na Ofisi ya Takwimu ya Kazi ya Marekani, wastani wa mshahara wa Marekani kwa wataalamu wa usimamizi wa miradi ni zaidi ya dola 94,000 sawa na Sh229,348,814 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Glassdoor, nchini Tanzania makadirio ya jumla ya malipo ya msimamizi mradi ni Sh4,210,900 kwa mwezi.

Mshauri wa Kazi (Consultant)

Mshauri wa kazi ni mtaalamu ambaye hutoa ushauri au huduma katika eneo la utaalamu. Huduma za ushauri kwa ujumla huwa chini ya kikoa cha huduma za kitaalamu, kama kazi ya dharura.

Wastani wa mshahara wa wa juu kwa mshauri wa kazi nchini Tanzania mwaka 2023 ni Sh25,919,400 kwa mwaka ambapo ni sawa na Sh2,159,950 kwa mwezi. Hii ni kwa mujibu wa tovuti ya World Salary.

Akili Bandia (Artificial Intelligence)

Kulingana na tovuti ya indeed Akili Bandia (AI), ni teknolojia inayoruhusu mashine kujifunza na kufanya maamuzi zenyewe. Ni fani inayokua kwa kasi inayotarajiwa kuendelea kupanuka katika miaka ijayo.

Kadiri teknolojia ya AI inavyoendelea kusonga mbele, ndivyo pia matumizi yake yanaziidi. Mnamo 2023, AI itatumika kufanya kazi na michakato kiotomatiki kabisa, kuboresha huduma kwa wateja, kuweka mifumo ya usalama kiotomatiki na mengine mengi.

Teknolojia ya AI inakuwa haraka kuwa ujuzi wa lazima kwa wataalamu katika tasnia nyingi huku kampuni zikizidi kutafuta watu ambao wanaelewa misingi ya AI na wanaweza kuitumia kuunda suluhisho kwa shida mahususi.

Ili kuwa mtaalam wa AI, lazima uelewe misingi ya programu, sayansi ya data na kujifunza kwa mashine. Kuwa na uelewa wa kina wa teknolojia za hivi karibuni za AI na matumizi pia ni muhimu. Ukiwa na ujuzi na maarifa sahihi, unaweza kuwa mtaalam wa AI na kujipatia mishahara mikubwa kwenye soko la ajira.

Anania Kapala anasema, hii ni teknolojia ya matumizi ya aina za roboti katika kufanya utambuzi sawa na mwanadamu ambayo kwa sasa inatumika maeneo mbalimbali zikiwamo taasisi za umma na hata za serikali.

Anasema kwa mtu anayetaka kuwa bobezi wa Akili bandia, anapaswa asome masomo ya geographic information system, GIS-AI yanayotolewa vyuoni na mitandaoni.

Kwa mujibu wa tovuti ya salaryexplorer, mtu anayefanya kazi hii nchini Tanzania kwa kawaida hupata takriban Sh1,550,000 hadi Sh2,410,000 kwa mwezi.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi