Connect with us

Kitaifa

Udhaifu mfumo wa haki jinai Tanzania huu hapa

Dar es Salaam. Tume iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini, imebaini kuwepo kwa mnyororo wa udhaifu katika mfumo mzima wa haki jinai.

 Hayo yameelezwa leo Jumamosi Julai 15, 2023 Ikulu Dar es Salaam wakati Tume hiyo ikikabidhi ripoti kwa Rais Samia.

Januari mwaka huu, Rais Samia aliunda Tume hiyo yenye wajumbe 11 wakiongozwa na Mwenyekiti, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Othman Chande huku Katibu wa Tume hiyo akiwa ni Balozi Omeni Sefue ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu.

Akiwasilisha ripoti ya Tume hiyo, Jaji Chande amesema udhaifu huo upo katika maeneo yanayo husika na kubaini na kuzuia uhalifu, kukamata na kupeleka watuhumiwa vituo vya polisi, uchunguzi na upelelezi wa makosa ya jinai.

Udhaifu mwingine ambao Tume imeubaini, upo kwenye masuala ya uandikishaji wa mashtaka, usikilizwaji wa kesi za jinai mahakamani na kwa watu waliotiwa hatiani na kutumikia vifungo gerezani.

Pia, Tume hiyo imebanini udhaifu kwenye makosa ya jinai na unaonekana hasa katika mfumo mzima wa kubaini wahalifu, kuwakamata na kuwapeleka watuhumiwa vituo vya polisi na gerezani.

Jambo jingine ambalo Tume hiyo imebaini halifanyiki kama inavyotakiwa, ni kuhusiana na masuala ya adhabu mbadala, maisha ya wafungwa wanapomaliza vifungo vyao na pale wanaporejea uraiani.

Jaji Chande amesema takwimu za uhalifu mkubwa za mwaka 2021/2022 zinaonyesha ongezeko la asilimia 9.8 ya uhalifu mkubwa ikiwemo mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha na utupaji wa watoto wachanga.

 “Tume imebaini kuwa hakuna mkakati wa kubaini na kuziuia uhalifu, ukosefu huo umesababisha vyombo vya utekelezaji wa sheria, kujikita zaidi kwenye ukamataji badala ya kuzuia uhalifu,” amesema Chande.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi