Kimataifa
Aokolewa chini ya kifusi vifo vikifikia 34,000 Uturuki, Syria
Dar es Salaam. Mwanamume mmoja ameokolewa kutoka kwenye vifusi karibu wiki moja baada ya tetemeko la ardhi la Jumatatu kusini mwa Uturuki na Syria.
Kwa mujibu wa BBC, Huseyin Seferoglu (23) alikuwa amenasa chini ya kifusi kwa siku sita na nusu, katika jiji la Antakya.
Seferoglu ameokolewa na vikosi vya uokoaji nchini Uturuki na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Waokoaji wameendelea kuokoa manusura zaidi kutoka kwenye vifusi nchini Uturuki na Syria huku idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea wiki iliyopita ikifikia 34,000.
Continue Reading