Kitaifa
Serikali yapendekeza mabachela kujisajili kwa Sh200,000
Dar es Salaam. Umewahi kujua kwamba ili utambulike rasmi kisheria kwamba haupo katika mahusiano kindoa ‘single’ unahitaji kuwa na cheti cha Serikali (Bachelor/Spinster Certificate) kinachotolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita)
Huduma hiyo ya utambuzi huo ambao hapo awali ilikuwa ikitolewa kwa gharama ya Sh100,000 kwa sasa itaanza kupatikana kwa kiasi cha Sh200,000 ifikapo Julai Mosi mwaka huu, nah ii ni kwa mujibu wa mapendekezo yaliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango ikiwa Bunge litaridhia.
Mapendekeo hayo yametolewa jana katika hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2023/24 bungeni jijini Dodoma.
Katika kiambatanisho namba 11 cha majedwali kimeonyesha namba ongezeko la asilimia 100 mpaka 1000 katika huduma mbalimbali ambazo hutolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA)?
Hata hivyo katika kiambatanisho hicho inaonyesha usajili wa talaka umeongezeka kutoka Sh20, 000 mpaka kufikia Sh40, 000.
Takwimu za Rita za mwaka 2020, zinaonyesha kuwa wakala ulisajili talaka 511 Tanzania nzima kati ya hizo 221 kutoka Dar es Salaam pekee.