Kimataifa
Majaliwa aanza na kamati waliyoomba wafanyabiashara
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameridhia ombi la wafanyabiashara waliotaka iundwe kamata ya kutatua kero zao wafanyabiashara itakayozunguka nchi nzima kukusanya kero hizo.
Kamati hiyo yenye wajumbe 14 inaundwa na wajumbe saba kutoka Serikalini na wajumbe wengine saba kutoka kwa wafanyabiashara. Kutoka serikalini itawajumuisha makatibu wakuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na makundi maalumu, Katibu Tawala Ofisi ya mkoa wa Dar es Salaam pamoja na TRA.
Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara hao amesema, “Nawaomba sana wafanyabiashara wetu mjue soko letu hili ni la Kimataifa, wale wateja walioondoka muwarudishe inaumiza kusikia vitenge vinashuka hapa kwenda Uganda na baadae kurudi nyuma nyuma,”amesema.
Jambo la pili Majaliwa amesema agizo lake la kuondoa kikosi kazi linabaki palepale kwani ilikuwa inafanywa na watu wenye tamaa za maisha akisisitiza kodi itakusanywa na watumishi wa TRA na watabanwa kulingana na maadili yao.
Pia amesema suala la Jeshi la Polisi kwenda kukusanya kodi linaleta mkanganyiko hivyo halipo na kuhusu kikosi kazi amekifuta kama alivyosema katika kikao cha awali kilichofanyika Mei 15, 2023.
“Kodi za stoo, kama inayotozwa na Wizara ya Viwanda na Biashara haina mgogoro kwanini hii ina mgogoro kuna tatizo mahala, Sheria iliyopo sio mbaya inawezekana kanuni ndio zinamianya ya kero hivyo kanuni hizo nazisitisha,”amesema.
Kuhusu mizigo iliyokamatwa Waziri Majaliwa ameagiza wote wenye mizigo watoe taarifa kwa kamati aliyounda ili uratibu wa kuipata mizigo hiyo uanze