Connect with us

Kitaifa

Serikali kununua meli kubwa za uvuvi

Dar es Salaam. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema ili kuimarisha uwezo wa uvuvi katika bahari kuu na taasisi za uvuvi ili kuongeza ushiriki katika Uchumi wa Buluu, Wizara imekusudia kununua meli za kuvua kwenye kina kirefu.

Ulega ameyasema hayo leo Jumanne, Mei 2, 2023 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2023/2024.

“Wizara kupitia programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi kwa ufadhili wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), inaendelea na taratibu  za ununuzi wa meli tatu za uvuvi wa bahari kuu  zenye vifaa vya kisasa kwa ajili ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).

“Hadi sasa, msawazo (Specifications) kwa ajili ya ununuzi wa meli hizo, upembuzi yakinifu wa awali (Pre-feasibility Study)  na andiko dhana umekamilika na kuwasilishwa kwenye mamlaka husika,” amesema Ulega.

Pamoja na hayo Ulega pia amesema mojawapo ya kipaumbele ni kuimarisha taasisi za uvuvi kwa kujenga miundombinu muhimu ikiwemo kununua boti mbili zenye vioo chini (glass bottom boat) ili kuongeza utalii kwenye hifadhi za bahari na maeneoTengefu.

Ulega amesema meli hizo pia zitatumika kufanya tafiti za kujua wingi, aina na mtawanyiko wa samaki katika maziwa ‘Victoria, Tanganyika, Natron na Eyasi). bahari ya hindi na bwawa la nyumba ya mungu; kujenga vyumba vitano vya mihadhara na vifaa vyakufundishia katika kampasi tano za FETA.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi