Kitaifa

Serikali yatangaza ajira mpya 2,611, nyingi za ualimu, omba hapa

Dar es Salaam. Serikali imetangaza nafasi 2,611 za ajira Februari 10, 2025 huku kati ya nafasi hizo asilimia 98 ni za walimu wa kada mbalimbali.

Katika tangazo hilo lililotolewa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma limesema mwisho wa kutuma maombi hayo ni Februari 20, 2025.

“Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi elfu mbili mia sita kumi na moja (2,611) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili,”imeeleza sehemu ya tangazo hilo.

Nafasi hizo ambazo kiwango kikubwa ni za ualimu, pia kada nyingine zipo kwa uchache ikiwamo zile za huduma kwa jamii na uhandisi.

Katika kada ya ualimu, maeneo yaliyotangazwa nafasi ni pamoja na: Mwalimu daraja la III C wa somo la biashara (2,316), mwalimu daraja la III B somo la ushonaji (18), mwalimu daraja la III B somo la uchomeleaji na utengenezaji wa vyuma (13), mwalimu daraja la III B somo la useremala (33) na mwalimu daraja la III B somo la huduma ya chakula, vinywaji na mauzo (28).

“Wengine ni mwalimu daraja la III B somo la upakaji rangi na uandishi wa maandishi (6), mwalimu daraja la III B somo la umeme wa magari (3), mwalimu daraja la III C somo la muziki (2), mwalimu daraja la III C somo la nishati ya jua (28).

“Mwalimu daraja la III B somo la uzalishaji wa chakula (14), mwalimu daraja la III B somo la ubaridi na mafriji (8), mwalimu daraja la III B somo la uchoraji wa kitekniki (2), mwalimu daraja la III B somo la uchoraji (2), mwalimu daraja la III B somo la uhandisi wa utengenezaji (2), mwalimu daraja la III B somo la bidhaa za ngozi na uzalishaji wa viatu (2), mwalimu daraja la III C somo la elektoniki na uhandisi wa mawasiliano (3), mwalimu daraja la III B somo la ujenzi wa majengo (1), mwalimu daraja la III B somo la fasihi ya Kiingereza (5), mwalimu daraja la III C somo la utengenezaji wa nguo (1) na mwalimu daraja la III C – somo la usanifu (17).

Kwa upande wa utawala na huduma za jamii jumla ya nafasi 101 zimetangazwa ambazo ni: Mwandishi mwendesha ofisi daraja la II (50) na mpishi daraja la II (51).

Pia, nafasi za afya na uhandisi  zimetangazwa katika kada mbalimbali ikiwamo: Daktari wa mifugo daraja la II (1) na msanifu majengo daraja la II (5)

Aidha, Sekreterieti ya ajira imesema waombaji wote watume maombi yao katika mfumo wa kieletroniki wa ajira (Recruitment Portal).

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi