Connect with us

Kitaifa

Mwenge kupandishwa Kilimanjaro

KILIMANJARO : WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Tanzania inapeleka mwenge wa uhuru juu ya mlima Kilimanjaro ili kuitangazia dunia kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni imara na pia utaendelea  kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Aidha, Waziri Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kwa mwaka huu 2024, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamuru mwenge wa uhuru upelekwe juu ya Mlima Kilimanjaro baada ya kuhitimisha mbio zake kwa siku 195.

Waziri amesema hayo katika hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakati wa hafla ya kupokea kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambacho kimepewa jukumu la kupeleka Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa ya Tanzania kilele cha mlima Kilimanjaro.

Awali Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema kupandishwa mwenge wa uhuru mlima Kilimanjaro mwaka huu 2024 kunaleta hamasa ya uzalendo kwa wananchi hususan wakati huu ambao Tanzania inaadhimisha miaka 60 ya uhuru na mafanikio ya Taifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia mwenge wa uhuru kupandishwa kwa mara nyingine katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Kiongozi wa mbio za Mwenge , Luteni Kanali Khalid amemhakikishia Waziri Ridhiwani Kikwete kuwa kikosi hicho kitafikisha kinaulinda na kuutunza Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa la Tanzania hadi katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi