Kitaifa
Wabunge wataka Serikali ikarabati barabara zilizoharibiwa na mvua
“Kamati inashauri Serikali ichukue hatua za dharura na madhubuti katika maeneo yaliyoharibika zaidi kutokana na mvua hizi, ikiwemo kufanya ukarabati wa haraka ili kupunguza athari na wananchi kukosa huduma,”amesema.
Aidha, Londo ameshauri Serikali kutumia bajeti ya dharura iliyotengwa kwa ajili ya kuendelea kukarabati maeneo ambayo miundombinu inaendelea kuharibika.
Amesema kamati haijaridhishwa na hali ya upelekaji wa fedha za bajeti kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura).
Amesema Serikali iliahidi ndani ya Bunge pamoja bajeti ya Sh808.02 bilioni ingetoa Sh350 bilioni za ziada kwa Tarura.
“Kamati inasikitika hata fedha hizi pia hazijapokelewa. Ni rai ya kamati kuwa Serikali ione umuhimu wa kuwapelekea Tarura fedha za kutosha kwa kadiri ya bajeti ilivyoidhinishwa na Bunge,” amesema.
Akichangia, Mbunge wa Viti Maalumu, Salome Makamba amesema kati ya Sh131 bilioni zinahitajika kwa ajili ya utengenezaji wa barabara zilizoharibiwa, ni Sh21 bilioni pekee ndizo zilipelekwa.
Akimpa taarifa, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Festo Dugange amesema kazi ya utengenezaji wa barabara zilizoharibika katika maeneo mbalimbali kutokana na mvua zinazoendelea.
“Kawe wamepata, Kibamba wamepata. Kwa hiyo nimuhakikishie kwamba pamoja kuna uharibifu mkubwa Serikali haijalala inaendelea kufanya matengenezo ya barabara hizo na hali itakwenda vizuri,”amesema.