Connect with us

Kitaifa

Miswada mitatu ya uchaguzi yatua kwa Spika

Dodoma. Wawekezaji wa kanda ya kati wametaja mambo matatu yanayotakiwa kufanyika ili kuongeza wawekezaji wa ndani,  ikiwemo upatikanaji wa taarifa sahihi kuhusu vivutio vilivyotolewa na Serikali.

Mengine ni unafuu wa kodi kwenye mikopo inayotolewa na benki pamoja na upatikanaji wa ardhi kwa bei nafuu.

Mmoja wa wawekezaji mkoani Dodoma, Peter Olomi ameyasema hayo mapema wiki hii, wakati akizungumza Mwananchi baada ya mkutano wa wawekezaji wa kanda ya kati ulioandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Amesema upatikanaji wa taarifa sahihi ambazo zimeshavunjwa vunjwa ni muhimu katika kuwawezesha Watanzania wengi kuelewa manufaa watakayoyapata kwa kuwekeza nchini.

Pia amesema jambo jingine ni kuwezesha upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji kwa bei nafuu, badala ya halmashauri nchini kutenga maeneo bila kuangalia gharama zake.

“Sasa hivi wanasema wametenga ardhi kwa ajili ya uwekezaji lakini gharama ya kununua  ikoje? Pia waongee lugha moja ukienda TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) mambo yawe wazi ni misamaha gani ambayo utapata,” amesema.

Amesema mitaji sio shida tena sasa kwa sababu benki nyingi zinatoa fedha, lakini inatakiwa kuwekwa riba maalum kwa wawekezaji kama inavyofanyika kwa nchi kama China.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA) mkoani Dodoma, Vivian Komu ameipongeza Serikali kwa kushusha kiwango cha mitaji ya uwekezaji ili kupata vivutio.

Amesema wafanyabiashara wanaweza kuchangia kiwango hicho cha Dola za Marekani 50,000 ili kunufaika na vivutio hivyo.

Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali Watu wa Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Benjamin Chilumba amesema mkutano huo unalenga kujengeana uwezo na  kutoa elimu juu ya maboresho ya sheria mpya ya uwekezaji, ambayo imepunguza kiwango cha chini cha mtaji ambacho mwekezaji wa ndani anatakiwa kuwa nacho ili kunufaika na vivutio.

Amesema sheria hiyo imeshusha kiwango hicho kutoka Dola za Marekani 100,000 hadi 50,000 kwa wawekezaji wa ndani.

“Hiki kilikuwa ni kilio kikubwa cha wawekezaji, sasa maboresho hayo yanatatoa fursa kwa wawekezaji wa ndani kuweza kuwekeza. Tumeongeza wigo wa vivutio kwa wawekezaji wa upanuzi na ukarabati hali hii itawezesha miradi inayotekeleza kupewa vivutio vya kikodi,”amesema.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa TIC, Shanilu Mayosa amewataka Watanzania kutumia fursa za uwekezaji zilizopo, na kwamba kituo hicho kiko kwa ajili kuwezesha Watanzania kuwekeza.

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi