Kitaifa

Rais apangua wakuu wa wilaya, wakurugenzi

Raymond Mwangwala aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro amepelekwa Wilaya ya Rombo.

Wakurugenzi waliohamishwa

Rais Samia amemhamisha Rose Manumba kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, huku aliyekuwa Mkurugenzi wa Malinyi, Rehema Bwasi akihamishiwa Mji wa Mbulu.

Yefred Myenzi, aliyekuwa Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Mbulu amepelekwa Halmashauri ya Mji wa Geita, huku aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Zahara Michuzi akipelekwa kuwa Mkurugenzi Ifakara.

Zahara anahamishiwa Ifakara kukiwa na uchunguzi dhidi yake kuhusu safari yake ya China.

Uchunguzi unafanywa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe uliolenga kubaini iwapo safari hiyo ilikuwa kwa masilahi ya halmashauri au binafsi.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mji Ifakara, Lena Nkya, amehamishiwa Halmashauri ya Mji Tunduma.

Rais amemhamisha, Chiriku Chilumba kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Kisena Mabuba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga,  huku Simon Berege akitolewa Shinyanga kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.

Michael Gwimile, amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Regina Bieda, amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Momba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, huku Mwajuma Nasombe akitoka Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

Aliyekuwa Mkurugenzi Manispaa ya Moshi, Rashid Gembe amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, huku aliyekuwa Mkinga, Zahara Msangi akihamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga.

 Mkurugenzi wa Mji Tunduma, Philemon Magesa amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, huku Butamo Ndalahwa aliyetoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha akipelekwa Wilaya ya Momba.

Taarifa hiyo inasema uteuzi na uhamisho huo umeanza Desemba 12, 2023.

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi