Makala
TUMUOMBEE SHANGAZI! KUNA JAMBO HALIKO SAWA, TAZAMENI HIZI PICHA MBILI!
Hapa ni Supermarket ya Carrefour Nairobi, na huyu ni shangazi Maria Sarungi. Shangazi alikimbilia Kenya wakati wa JPM na mpaka leo kajichimbia huko huko. Habari za ndani zinasema hata baada ya Samia kuingia madarakani shangazi kaamua kubaki Nairobi kwa sababu uanaharakati wake unampa fursa kupata mamilioni kutokana kwa Bilionea wa Kimarekani, George Soros. Akirudi Tanzania itaonekana nchi iko salama kwake kuendelea na maisha na hatapata tena fedha hizo za Soros.
Sasa tuachane na hayo kwanza, ninachowaomba ndugu zangu ni kumuombea shangazi. Nimekutana naye leo asubuhi hapa kwenye hii supermarket, sio shangazi yule niliyemfahamu. Mwili umekuwa mkubwa sana, sura imedhoofu na wapo wanaosema ana ugonjwa mkubwa na inabidi kutumia madawa makali ambayo yameathiri afya yake kiasi hiki.
Maisha yake ya Nairobi pia si mazuri. Amekuwa mtu wa hofu kubwa, anaishi ndani muda mwingi isipokuwa akitoka kununua mahitaji kama hivi jambo ambalo limempa msongo mkubwa wa mawazo. Kuna taarifa kuwa kutokana na ugonjwa unaomkabili anatakiwa kupumzika zaidi jambo ambalo ameendelea kutozingatia na hivyo kusababisha afya yake kuzorota.
Natoa wito kwa Watanzania bila kujali dini wala chama, kumuombea sana. Kwanza aweze kurudi nyumbani ambako kwa kweli hali si mbaya ikiwa hadi Lissu karudi na anafanya mikutano bila wasiwasi. Pili aweze kurudi kwenye shughuli zake za kumuingia kipato kama kampuni yake ya urembo na mawasiliano. Hii itamsaidia kuachana na kazi hii ya aibu anayofanya kwa sasa ambayo ili ulipwe lazima kuonesha kwenu hakuko salama. Kila siku kutengeneza habari ambazo wakati mwingine hazina uhalisia wowote ili tu kuonesha kwenu kuna moto na inabidi usaidiwe na kulipwa kuishi uhamishoni kufanya harakati. Nafahamu baadhi yenu mmeanza kumpuuza na kumuona ni mpiga kelele anayelipwa na wageni na taasisi za kimataifa lakini kwenye hili la afya yake ya mwili na akili, chondechonde tumsaidie kwa maombi.