Connect with us

Kitaifa

Dk Tulia ashinda kwa kishindo urais IPU

Da es Salaam. Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amefanikiwa kushinda uchaguzi wa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), uliofanyika leo Luanda nchini Angola.

 Dk Tulia amewabwaga Adji Diarra Mergane Kanouté, (Senegal), Catherine Gotani Hara (Malawi) na Marwa Abdibashir Hagi (Somalia).

Mshindi huyo atachukua nafasi inayoshikiliwa na Duarte Pacheco, ambaye ni Spika wa Ureno, aliyechaguliwa mwaka 2020 wakati wa mlipuko wa Uviko-19 na sasa amemaliza muda wake.

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi