Connect with us

Kitaifa

Rais Samia ateua bosi mpya wa TPHPA

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteuwa Profesa Joseph Ndunguru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA).

Taarifa ya uteuzi huo, imetolewa leo, Oktoba 24, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Ndunguru alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu February mwaka huu.

Kabla ya hapo, Profesa Ndunguru alikuwa Meneja wa Utafiti wa Kilimo (Tari) Kituo cha Mikocheni jijini Dar es Salaam.

TPHPA ndiyo inayohusika na udhibiti wa viuatilifu na kuhakikisha afya ya mimea katika mazao ya kilimo.

Oktoba 11, mwaka huu Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde alisema mpango wa Serikali ni kuitumia TPHPA kuhakikisha usalama wa chakula nchini.

“Uimarishwaji wa TPHPA ni moja ya vipaumbele vya wizara katika kuhakikisha mauzo ya mazao nje ya nchi yanaongezeka kutoka Dola za Marekani 1.2 bilioni hadi kufikia Dola za Marekani 5 bilioni kupitia huduma bora za ukaguzi za mamlaka hiyo,” alisema Silinde.

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi