Connect with us

Makala

Ukakasi wa malipo ya Barrick/Acacia kwenda Task Force ya Serikali mwaka 2014 hadi 2019

Wiki hii gazeti la Uingereza la Global & Mail limechapisha barua pepe zaidi ya 100 kuhusu Tanzania. Barua pepe hizo zinaonesha namna Barrick Gold kupitia kampuni yao ya Tanzania Acacia walivyolipa mabilioni ya shilingi kwa kinachoitwa kikosi kazi cha Taifa Tanzania kama gharama za ulinzi, mpokeaji mkuu akiwa IGP.

Malipo hayo yamefanyika kati ya mwaka 2014 hadi 2019. Hakuna chombo cha habari Tanzania kiliwahi kuchapisha taarifa hiyo. Uingereza taarifa hii imechapisha baada ya sehemu yake kutakiwa kwenye kesi nyingine mahakamani nchini humo.

Taarifa hii imenifanya nijiulize maswali kadhaa

1. Malipo yamefanyika kuanzia 2014 hadi 2019, Marais waliokuwepo madarakani (Kikwete & Magufuli) walifahamu? Walibariki?

2. Utaratibu huu wa wawekezaji kulipa serikali kwa ulinzi wa ziada ni wa kawaida? Wanalipa wawekezaji wote? Kwamba mbali na kodi pia kuna malipo ya kisiri ya ulinzi wa ziada?

3. Kama sio sawa, ilikuwaje vyombo vyetu vya habari havikuwahi kubaini na kutoa taarifa hizi? TAKUKURU je? Tanzania hatuna tena vyombo vya habari vya kiuchunguzi?

4. Pesa hii ya ulinzi wa ziada kama ni sahihi ilikuwa inakwenda wapi? Kwa viongozi wa juu au kwa askari wa chini ambao kimsingi ndio wanaifanya kazi?

Nazidi kuona umuhimu wa Tume aliyounda Rais Samia kuleta maboresho ya utendaji wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na vile vya haki jinai. Anaweza kupitia wakati mgumu kujaribu kubadili baadhi ya mifumo ya namna hii lakini imani yangu ni kuwa atafanikiwa. Ni wakati sasa vyombo vyetu vya habari pia kujitazama kwamba habari muhimu kama hizi tunazipata kutoka vyombo vya nje badala ya ndani.

Tanzania Itadumu!

Ndugu yenu
Faraji Kanuni
Mara

Continue Reading

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi