Connect with us

Kitaifa

Watu milioni 9 walioandikishwa kupatiwa vitambulisho Machi mwakani

Dodoma. Hadi kufikia Julai 31, 2023 jumla ya Watanzania 11,242,736 walikuwa wamepewa vitambulisho vya Taifa. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 55 ya lengo la kuwapatia 20,294,910 wanaostahili kupewa.

 Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Jumatano Septemba 6, 2023 na Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais, Khamis Hamza Chilo kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Chilo alikuwa akijibu swali lililoulizwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Matiko aliyeuliza ni asilimia ngapi ya Watanzania wameandikishwa na kupatiwa Kitambulisho cha Taifa.

Naibu Waziri amesema kwa sasa mpango wa Serikali ni kuwagawia vitambulisho Watanzania 9,052,174 waliobaki ifikapo mwezi Machi, 2024 kwani mipango yote imeshakamilika.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi