Makala
Ushuhuda na maoni ya mdau wa biashara ya mafuta
Na Hakim Maneti, DSM
Katika sakata la mafuta nimegundua yafuatayo.
1. Mafuta yapo, wanaoleta shida ni wenye vituo kuzuia kuuza stock ya mafuta wakisubiri bei mpya iende juu ili faida yao iwe kubwa.
2. Serikali ifanye msako na kutoa adhabu kwa vituo vinavyofanya ghasia hii kwa sababu ni uhujumu uchumi.
3. Inawezekana pia vituo hivi vinatumiwa na wapinzani au mataifa ya nje kuleta taharuki kwenye siasa za ndani na utulivu wa nchi yetu hivyo mbali na adhabu wamiliki wamulikwe zaidi mara kwa mara.
4. Suala la utoaji wa leseni za vituo vya mafuta litazamwe kama suala la uhai na usalama wa nchi. Kama ambavyo tunatumia muda mwingi kufanya vetting ya leseni za makampuni ya mbegu za mimea yanayokuja nchini, NGOs, leseni za benki n.k. umefika wakati sasa kuwa na utaratibu makini zaidi kutoa leseni za wafanyabiashara ya mafuta ili kuzuia uhujumu tunaouona mara kwa mara.