Kitaifa

Samia anyooshea kidole rushwa kwa polisi

Akizungumza leo Jumatatu Septemba 4, 2023 wakati wa ufunguzi wa kikao cha maofisa waandamizi wa jeshi la polisi Rais Samia amesema wananchi bado wanalalamikia rushwa hasa kwa askari wa barabarani.

“Wimbo wa polisi mzuri na leo kabla ya kuja hapa nilifungua youtube nikausikiliza kisha nikaangalia jeshi langu na kujiuliza ingekuwa yanayoimbwa hapa ndiyo yanayotendeka tungekuwa na jeshi la malaika.

Ukiachana wimbo na slogan yenu nzuri sana lakini je mnayatekeleza? IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi) naomba sana simamia utekelezaji wa wimbo na slogan ili jeshi liwe na sifa ile ya kimataifa,” amesema Rais Samia.

Hata hivyo amebainisha kuwa tatizo la rushwa kwa askari wa barabarani litapatiwa ufumbuzi baada ya uwekezaji kufanyika kwenye teknolojia.

“Wakati mwingine ni vigumu kubadilisha tabia lakini inaweza kurekebishika kukiwa na teknolojia inayolazimisha watu wafuate teknolojia inavyotaka.

“Mfano tukiweka kamera za barabarani hakutakuwa na sababu ya askari kusimama barabarani kusimamisha magari teknolojia itatoa mwongozo wa kila kitu na rushwa haitakuwepo,” amesema.

Rais Samia amefafanua uwekezaji huo ukifanyika kwenye teknolojia itasaidia kupunguza idadi ya askari barabarani na itawezesha kupatikana wa kwenda kwenye maeneo mengine yenye uhitaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi