Connect with us

Kitaifa

Kwa nini mikutano ya hadhara ya CHADEMA inaendelea kupata watu wachache siku hadi siku?

Na Dr. George Mayala
Nyegezi Mwanza

Januari mwaka huu Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitangaza kuruhusu mikutano ya hadhara ya kisiasa. Mikutano hiyo ilikuwa imepigwa marufuku (kinyume na Katiba ya Tanzania) na mtangulizi wake hayati Rais Dkt John Magufuli.

CHADEMA, moja ya chama kikongwe cha upinzani Tanzania kilianza mkutano wake wa kwanza kwenye Jiji la Mwanza. Hata hivyo baada ya mkutano huo, mikutano iliyofuata imekuwa ikishuhudia mwitikio mdogo wa watu na wakati mwingine kulazimika kuahirisha mikutano. Bwana Chris Mageni ni mtaalamu wa Sayansi ya Siasa toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ana ametaja sababu kadhaa za hali hii kama ifuatavyo:

1. Usingizi wa harakati. Bwana Mageni anaeleza kuwa kwa miaka sita ya marufuku ya mikutano hii chini ya Magufuli, baadhi ya wananchi ni kama bado wako usingizini linapokuja suala la masuala ya harakati za kisiasa na hali hii inachangia mahudhurio machache kwenye mikutano ya CHADEMA.

2. Ujasiriamali wa kisiasa. Kuanzia mwaka 2015 baada ya kumpokea Edward Lowassa kumekuwa na tuhuma nyingi kwamba chama hicho kilinunuliwa na mwanasiasa huyo tajiri. Wandani wa CHADEMA wanasema fedha alipokea Mbowe na kukawa na mvurugano mkubwa uliosababisha baadaye Dr Slaa kuondoka. Wachambuzi wanasema kitendo hiki kinawapa baadhi ya wananchi picha kuwa hiki si chama hasa chenye itikadi bali nafasi ya baadhi ya viongozi wake kufanya biashara.

3. Kukosa itikadi na sera mbadala. Kwa muda mrefu kimeonekana kuwa chama cha matukio. Kazi zake na matamko yake mengi yamekuwa yakifanyika kuendana na upepo wa siku au mwezi. Kwa miaka 31 CHADEMA kimekuwa chama cha upinzani na mwenendo wake huu ni kama wananchi wameanza kuuchoka kwa kutokuwa na sera mbadala na kuishi kwa upepo wa matukio.

4. Rushwa na ufisadi. Katika taarifa mbalimbali za miaka zaidi ya 15 sasa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali amekuwa akiibua madudu kwenye hesabu za vyama namna wanavyotumia ruzuku ya serikali. Pamoja na mambo mengine CAG ameonesha namna mabilioni ya fedha yanavyotumika na kikundi kidogo cha chama hicho kujineemesha ikiwemo kujinunulia magari, mali na starehe. Wananchi wengi wanasema hii haipaswi kuwa sifa ya chama kinachojinasibu kuwa cha ukombozi na hii ni hadaa.

5. Udini, ukabila na utawala wa kiimla. Kamati Kuu ya CHADEMA ina picha ya kitaifa kama geresha lakini bado maamuzi mengi yanafanywa na watu wa Kanda ya Kaskazini. Mbowe amekuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka zaidi ya 15 sasa na ni mkwe wa mwanzilishi wa CHADEMA. Kukosa uwiano wa kidini pia kunatajwa kwani zaidi ya 75% ya viongozi waandamizi ni Wakristo.

Wachambuzi wengi wa siasa wanasubiri kuona nini kitatokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025. Kwa mwenendo wa siasa za upinzani Tanzania ukianzia ufinyu wa mahudhurio kwenye mikutano yao, kuna kina dalili Rais Samia na chama chake cha CCM kupata ushindi mkubwa wa kuendelea kuiongoza Tanzania.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi