Kitaifa
RAIS SAMIA SIO DHAIFU NI IMARA KULIKO WATANGULUZI WAKE NA HIZI NI SABABU ZANGU
Na Thadei Ole Mushi
Ndiye Rais ambaye unaweza kumwambia akili zake ni matope lakini bado akavumilia na ukaendelea kula Ugali wako Uraiani.
Ndiye Rais Ukanda huu wa Africa unaweza kumwambia anafuga wezi na akakuacha ukaendelea kula ugali wako Uraiani.
Ndiye Rais ambaye baada ya Kuingia madarakani aliwaondolea watumishi kifungo cha kutokupanda madaraja kwa wakati na sasa kila mtu anapanda kila anapostahili.
Ndiye Rais ambaye aliwafungulia kina Mbowe account zao zilizokuwa zimefungwa na kuwarejeshea haki zao.
Ndiye Rais ambaye Alihakikisha Lisu amepata haki yake ya kutibiwa na haki zake za kibunge alizokuwa amedhulumiwa.
Ndiye Rais ambaye amekubali kuwaita wapinzani Ikulu na kuongea nao kuhusu mambo mbalimbali ya Kisiasa nchini hapo kabla hili halikuwezekana.
Ndiye Rais anayejitahidi kuajiri kuliko Marais wengine wote waliomtangulia.
Ndiye Rais ambaye kuingia kwake madarakani hakutaka kuanzisha miradi yake anapambana kukamilisha miradi yote ya Mtangulizi wake kwa mara ya kwanza tunaona Continuity kati ya Rais mmoja na mwingine.
Ndiye Rais aliyevitoa vyombo vyote vya habari Gerezani na kuviruhusu kuandika wanavyotaka.
Ndiye Rais aliyehakikisha waliokuwa wametupwa lupango kwa sababu za kisiasa na kiuchumi kama kina mzee Rugemalila wanatoka na wapo uraiani.
Ndiye Rais ambaye anapambana Sector Binafsi itoke ilikokuwa imefukiwa ifanye kazi sambamba na serikali.
Ndiye Rais ambaye hakusanyi kodi kwa kutumia kikosi Kazi wala mabavu.
Ndiye Rais ambaye kuingia kwake madarakani wasiojulikana nao walikwenda kusikojulikana.
Ndiye Rais ambaye alitufutia Retention Fee sisi wanufaika wa Bodi ya Mikopo na mikopo yetu kumalizika kwa wakati.
Ndiye Rais ambaye ameweza kuleta tofauti ya maendeleo ya vitu na watu kwa kusogeza huduma za kijamii kadri anavyoweza kwa wananchi.
Ndiye Rais aliyefuta ada kwa vidato vya tano na Sita.
Ndiye Rais ambaye amepandisha kiwango cha fedha za wanufaika wa Mikopo na kuongeza wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.
Ndiye Rais nwenye uwezo wa kuhimili wakosoaji wake kuliko watangulizi wake.
Ameichukua nchi ikiwa imetoka kwenye Wimbi kubwa la Corona ila Uchumi haukuyumba, wananchi hawakukosa chakula ulizeni majirani athari za Corona watawaambia.
Kwenye miundombinu ya Barabara, Madarasa, Vituo vya Afya na Huduma za Maji safi na Salama amevunja Rekodi.
Binadamu tuna tabia za kusahau, kwa sasa tushasahau yote haya, huyu ndiye Rais tunayetakiwa tumeombee adumu nasi. Huyu ni mama haswa. Sio mtu dhaifu, mtu dhaifu hana uwezo wa kuvulia hivyo, kupitia taasisi yake anaweza kufanya mengi kama ambavyo watanguluzi wake walifanya. Kuna siku tutamtafuta kiongozi kama huyu tutamkosa.
Ni miaka miwili tu madarakani lakini katurudishia kila kitu tulichopoteza.