Kimataifa

Rais Ruto wa Kenya, akubali kukutana na Raila

Dar es Salaam. Rais wa Kenya, William Ruto, ameweka wazi utayari wake wa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Kiongozi wa Upinzani nchini humo, Raila Odinga, katika jitihada za kumaliza maandamano ya kuipinga Serikali ambayo yamekuwa yakitiitishwa na upinzani.

Ruto ameyasema hayo ameyasema hayo jana Julai 25, 2023 kwenye ukurasa wake wa X (Twitter), kwamba yupo tayari kuonana na Odinga mara tu atakaporejea akitokea Tanzania, kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu rasilimali watu.

Katika ujumbe huo, Rais huyo wa Kenya amebainisha kuwa atarejea nchini humo leo jioni na kwamba muda wowote yuko tayari kukutana na kiongozi huyo wa upinzani.

Hatua hii inakuja baada ya miezi kadhaa ya maandamano ya kuipinga Serikali ambayo yamezua taharuki kubwa kitaifa na kimataifa.

Tangu kuapishwa kwake Septemba 13, 2022 kama Rais wa Jamhuri ya Kenya, Serikali ya Ruto imekuwa ikikumbwa maandamano ya mara kwa mara ya upinzani, yanayotoishia kuitumbukiza nchi hiyo katika machafuko.

Awali Serikali ilibainisha kuwa mazungumzo yeyote baina ya hizo pande hizo mbili, yangefanyika kupitia wabunge wao (Bungeni) na kwamba hakutakuwa na mambo ya kugawana madaraka wala kushikana mikono (handshake) kama ilivyotokea katika utawala uliopita.

Ofa hiyo ya mazungumzo imetolewa muda mfupi baada ya Odinga kuimshutumu Serikali kwa kumsubirisha Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassa, ambaye aliwasili nchini humo wiki mbili zilizopita, akiwa na lengo la kupatanisha mzozo unaohusishwa na kupanda kwa gharama za maisha na uchaguzi.

Kwa mujibu wa Odinga, Rais Samia ambaye alitaka kufanya suluhu kupitia mazungumzo baina ya pande mbili zenye mzozo(Kenya Kwanza na Azimio), nia hiyo haikutimia kwa kile inadaiwa Serikali haimkumpa ushirikiano kwa siku mbili alizokuwepo nchini humo.

“Aliendelea kusubiri. Tulikuwa tunapatikana lakini kundi lingine halikuwepo. Suluhu alikaa hapa kwa siku mbili lakini yote yalikuwa bure,” Odinga aliwaambia waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya kimataifa jijini Nairobi Jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi