Connect with us

Kitaifa

Abiria wanusurika kifo, basi likizama kivukoni Pangani

Pangani. Sheria iliyowekwa na Serikali ya watu kushuka kwenye magari wakati yanapovushwa na vivuko umewanusuru abiria wa basi la Kampuni ya Moa lililozama leo mchana katika Mto Pangani.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa  na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe, basi hilo lililokuwa likitokea jijini Tanga kuelekea Kipumbwi wilayani Pangani  limezama baada ya kushindwa kupanda kilima cha Bweni na kisha kurudi nyuma hatimaye likakigonga kivuko cha MV Pangani na kutumbukia majini.

Watu waliishuhudia tukio hilo wamesema basi hilo lilikuwa likrudi taratibu baadaye walimuona dereva akiruka likagonga upande wa kushoto wa kivuko na kuingia majini.

“Lilikuwa likirudi kinyumenyume tukashangaa kwa sababu siyo kawaida baadaye tukaona dereva anaruka ghafla likagonga kivuko na kuingia majini” amesema Fatuma Charles mkazi wa Pangani Mashariki mjini Pangani.

Meneja wa Vivuko wa Wakala wa mitambo (Temesa) kanda ya Kaskazini, Likombe King’ombe amesema matumizi ya sheria inayoamuru kila gari linalovushwa lazima abiria kushuka yamewanusuru abiria wa basi la Moa kuzama.

“Kuna wakati hata viongozi wanapovushwa baadhi yao huwa hawatuelewi tukiwaambie washuke kwenye magari ni mambo kama haya yakitokea hatari ni kubwa” amesema King’ombe.

Hata hivyo Meneja huyo amesema licha ya kuwa kivuko cha MV Pangani kimegongwa pembe ya upande wa kushoto lakini  haijaharibika na inaendelea kutoa huduma kama kawaida.

Pia, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah amefika eneo la tukio na amesema hakuna aliyepoteza maisha wala majeruhi kwenye ajali hiyo.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Telephone: +255 653 313 586 | Email: mhariri@chechetimes.com. | Address: 14216 Keko Magurumbasi